Rais wa Guinea Bissau amekutana na Felix Tshisekedi jijini Kinshasa

Rais wa Guinea Bissau, Umaro Sissoco Embalo, yuko katika ziara ya kikazi ya siku mbili nchini DRC ambapo aamekutana kwa mazungumzo na mwenyeji wake rais Felix Tshisekedi na kujadiliana kuhusu masuala ya kidiplomasia, uchumi na usalama.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Baada ya rais Tshisekedi na mwenzake wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco kufikiana kuhusu suala la kufungua ubalozi wa mataifa hayo mawili Kinshasa na Guinea, marais hawa walijadili pia hali ya usalama mashariki mwa DRC. Umaro akisema, ataendelea kujiusisha katika utafutaji wa amani eneo hilo la DRC.

“Hakika nilikutana na Rais Kagame, tulijadiliana sana kuona namna gani tunaweza kupata amani kati ya nchi hizi mbili na Rais Felix pia. Licha ya kwamba sijapewa jukumu lakuwa mpatanishi wa nchi hizi, jambo pekee ninaloweza kuleta ni urafiki wangu.” Alisema rais Umaro Sissoco.

AKizungumzia hadharani kwa mara ya kwanza kuhusu mkataba ulioafikiwa kuelekea njia kuelekea makubaliano ya amani kati ya DRC na nchi ya Rwanda, rais Felix Tshisekedi, alisema:

“Mkataba huo ni hatua katika mwelekeo sahihi, mwelekeo ambao siku zote nilitaka kuweka katika nchi yangu. Nilitoa ahadi hii mbele ya raia wangu na nitatimiza, “nitaleta amani ya kweli na yakudumu. Baada ya kile munachokiona, hakutakuwa tena na tatizo la ukosefu wa usalama nchini DRC. Alisema rais Félix Tshisekedi.

Siku ya Ijumaa, Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka DRC na Rwanda, walitia saini mkataba wa kila nchi kuheshimu mipaka ya mwenzake, na kuendeleza mashauriano ya kumaliza tofauti zao, miongoni mwa mambo mengine.

Freddy Tendilonge/Kinshasa/RFI Kiswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *