Ubelgiji inaitaka Kinshasa kutoa kipaumbele kwa mazungumzo ya kitaifa

Ubelgiji inaitaka serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kutoa kipaumbele kwa mazungumzo ya kitaifa, kama inavyoendekezwa na viongozi wa dini, ili kupata suluhu ya changamoto za usalama Mashariki mwa nchi hiyo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Wito huo umetolewa na Maxime Prévot, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya nje wa Ublgiji, baada ya kukutana na rais Felix Thisesekedi kwenye mazungumzo ya ana kwa ana siku ya Jumatatu, jijini Kinshasa.

Prévot, amesema pamoja na jitihada za kikanda na Kimataifa kupata suluhu, ni muhimu kwa serikali ya DRC kutanguliza mazungumzo ya kitaifa, kama inavyopendekezwa na Kanisa Katoliki na viongozi wa madhebu mengine  ili kupata suluhu.

Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki CENCO na Kanisa la Kristo nchini Congo-ECC kwa pamoja zinaongoza uhamasishaji wa mazungumzo hayo ya ndani na hata, wawakilishi wake wamekutana na wawakilishi mbalimbali, wakiwemo viongozi wa nchi mbalilmbali za kikanda kutafuta uungwaji mkono.

Mchakato huu umeonekana kutoungwa mkono na serikali, lakini wapinzani nchini humo wameukubali. Rais Tshisekedi, amekuwa akionelea kuwa kazi ya kuleta amani Mashariki mwa nchi hiyo, ifanywe na watu wa nje, na viongozi wa dini wasijihusishe na masuala ya siasa.

Licha ya serikali ya DRC kukubaliana na waasi wa M23 kuendeleza harakati za kuleta amani baada ya mazungumzo ya Doha, lakini pia serikali ya Kinshasa na Kigali kutia saini mkataba nchini Marekani kukubaliana kuanza kurejesha tena uhusiano wao na kusaidia kuleta amani, vita vimeripotiwa tena huko Kivu Kaskazini na Kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *