DRC: Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji akutana na Félix Tshisekedi mjini Kinshasa

Baada ya kuzuru Uganda na Burundi, Naibu Waziri Mkuu wa Ubelgiji na Waziri wa Mambo ya Nje, Maxime Prévot, amehitimisha ziara yake katika eneo la Maziwa Makuu nchini DRC. Jumatatu, Aprili 28, mjini Kinshasa, amekutana na Waziri Mkuu wa Kongo, Judith Suminwa, na kisha na Rais Félix Tshisekedi, ambaye amejadiliana naye kuhusu mgogoro kati ya DRC na Rwanda.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa Kinshasa, Pascal Mulegwa

Wakati wa awamu ya mwisho ya ziara yake katika eneo la Maziwa Makuu mjini Kinshasa, Naibu Waziri Mkuu wa Ubelgiji na Waziri wa Mambo ya Nje wamejadili vita mashariki mwa DRC na Waziri Mkuu wa Kongo Judith Suminwa na Rais Félix Tshisekedi.

Ingawa alikuwa amekaribisha mipango ya Qatar na Marekani katika suala hili, ambayo yaliwezesha kufikia makubaliano kimsingi kati ya Kinshasa na waasi wa M23 kwa upande mmoja, na Kinshasa na Kigali kwa upande mwingine, Maxime Prévot hata hivyo alitmia fursa ya ziara yake katika mji mkuu wa Kongo ili kurejesha wito wake wa tahadhari.

“Lazima tuwe macho kuhusiana na michakato iliyoanzishwa na Doha na Washington. Ingawa tuna maoni chanya kuhusu mapokezi ya mipango hii, tunataka hasa kuwa na uwezo wa kupima matokeo madhubuti yanayoweza kutokea katika siku au wiki zijazo, ili kuhakikisha kwamba ikiwa barbara itakuwa imetengenezwa, itaendelea kutumika, na kwamba hakutakuwa na mashimo mengi sana kwenye barabara hiyo na kwamba hatua ya mwisho itatangazwa.”

“Niliomba wadau wasikilize mpango wa maaskofu”

Wakati wadau wa kisiasa wengine wa kimataifa wana, kulingana naye, “mbinu ya kimaadili zaidi kwa diplomasia yao”, Brussels haitaki “kuchimba” rasilimali za Kongo, ameendelea Maxime Prévot, ambaye pia amemtaka Rais Tshisekedi kutopuuza mipango ya ndani katika kutatua mgogoro.

“Tunafahamu kwamba ni muhimu kwamba ishara itolewe na mazungumzo ya kitaifa yaendelezwe, pia yasaidie utatuzi wa migogoro na kutetea amani. Kwa hiyo, naomba kuwe na umakini wa kujitolea, muweze kusikiliza mpango wa maaskofu kwa kuongeza nguvu mbalimbali za kisiasa zilizopo kwenye meza,” amebainisha wakati huo huo, alitoa maelezo hayo wakati maaskofu na wachungaji wa makanisa ya Kikatoliki na Kiprotestanti walipokelewa na mkuu wa diplomasia ya Qatar…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *