
Mali, Niger, na Burkina Faso hazina bahari. Kwa miezi kadhaa, wamekuwa wakivutiwa sana na mpango uliozinduliwa na Morocco ambao ungewapa ufikiaji wa Bahari ya Atlantiki. Ni katika hali hiyo ndipo mawaziri wa mambo ya nje wa Mali, Nigeria na Burkina Faso walisafiri jana (Jumatatu) kwenda Rabat ambako walithibitisha ahadi yao ya kuharakisha utekelezaji wa mradi huu.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali Abdoulaye Diop, Waziri wa Mambo ya Nje wa Niger Bakary Yaou Sangaré na waziri wa mambo ya Nje wa Burkina Faso Karamoko Jean-Marie Traoré walikutana jana, Jumatatu, Aprili 28, mjini Rabat na Mfalme Mohammed wa Sita.
Picha ya mkutano huo ilikuwa ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii siku ya Jumatatu jioni. Watatu hao, kulingana na shirika la habari la Morocco, walikaribisha mpango uliozinduliwa na Mohamed VI, “wakithibitisha uungwaji mkono wao kamili na kujitolea kwao kuharakisha utekelezaji wake.” Mradi huu wa kufikia Bahari ya Atlantiki ulitangazwa mnamo mwezi wa 2023 na Mfalme wa Morocco. Mkutano wa kwanza uliandaliwa huko Marrakech na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizi nne.
Kuchochea mvutano na Algiers
Je, Sahara Magharibi inahusika na mradi huu? Bahari ya Atlantiki inaenea kando ya pwani ya eneo hili linalozozaniwa linalodaiwa na Polisario Front, vuguvugu linalodai uhuru linaloungwa mkono na Algeria. Mpango huo kwa hivyo unahatarisha kuchochea zaidi mvutano kati ya Algiers, Rabat na nchi za ESA. Akihojiwa na RFI mnamo mwezi wa Desemba 2023, mtafiti Youssef Chiheb, profesa katika Chuo Kikuu cha Sorbonne Paris Nord, aliangazia mwelekeo huu wa kisiasa wa kijiografia kwa mpango ambao “ni sehemu ya ushindani wa muda mrefu na wenye misukosuko kati ya Morocco na Algeria kwa nafasi za uongozi barani Afrika na haswa Kusini mwa Jangwa la Sahara, Sahel na Sahara,” amesema.
Lakini kwa nchi hizi tatu zisizo na bandari, mradi huo ni muhimu, wakati ambapo mataifa haya, yanayotawaliwa na wanajeshi, mara nyingi yanadumisha uhusiano mbaya na nchi za Ghuba ya Guinea.
Mkuu wa Diplomasia ya Niger jana aliuelezea mpango huo kuwa ni “unastahiki”. Lakini mpango ambao unaweza kuchukua muda kutekelezwa: hakuna ratiba ambayo imetangazwa kwa utekelezaji wake…