Ufaransa yaitaka Israeli ‘kusitisha mauaji yanayotokea leo Gaza’

Ufaransa inatoa wito kwa Israeli “kusitisha mauaji yanayotokea leo huko Gaza,” msemaji wa serikali Sophie Primas amesema siku ya Jumatatu, Aprili 28, kulingana na shirika la habari la AFP.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Sophie Primas amefafanua kwa vyombo vya habari kwamba Paris pia inadai kuachiliwa kwa mateka ambao bado wanashikiliwa na Hamas katika eneo hilo, na “kuondolewa kijeshi” kwa vuguvugu la Kiislamu la Palestina linalodhibiti eneo hilo, pamoja na “kuanzishwa upya kwa Mamlaka ya Palestina.”

Kulingana msemaji wa serikali, haya ni “masharti ya kuelekea kutambuliwa” kwa taifa la Palestina, ambalo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekusudia mwezi Juni 2025.

Majadiliano juu ya mfululizo wa utambuzi “yanasonga mbele”

Rais wa Ufaransa anatarajiwa kuwa mwenyekiti mwenza wa mkutano wa kimataifa katika Umoja wa Mataifa mwezi Juni na Saudi Arabia kuzindua upya suluhisho la mataifa mawili ya Palestina na Israeli.

Sophie Primas anatumai katika hafla hii “kuanzisha safu ya kutambuliwa” kwa taifa la Palestina, haswa na Ufaransa, lakini pia kwa Israeli na nchi kadhaa katika ulimwengu wa Waarabu-Waislamu.

“Nadhani majadiliano yanaendelea, kwa hakika, hatuyatangazi kila asubuhi kwa sababu haya ni mambo nyeti sana, muhimu sana,” amesema Sophie Primas kuhusu mazungumzo ya kuelekea mkutano huu wa mwezi Juni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *