Makadinali wa kanisa katoliki, Jumatatu ya wiki hii walikubaliana tarehe 7 ya mwezi ujao kuwa tarehe rasmi kuanza vikao vya baraza la siri kuelekea kuchagua papa mpya.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Makadinali walio na umri wa chini ya miaka 80 watakutana katika kanisa la Sistine kuchagua papa mpya atakayeongoza waamini zaidi ya bilioni 1.4 duniani kote, uchaguzi ambao ikiwa kiongozi mpya atapatikana atakabiliwa na mlima wa chagamoto zilizoachwa na mtangulizi Wake.
Baada ya kifo cha Papa Francis, Makadinali 252 waliitwa, ingawa ni 135 tu ndio wanastahili kupiga kura, 108 kati yao walichaguliwa na Papa Francis.

Kwa mujibu wa utaratibu wa uchaguzi wa papa, zitapigwa kura nne, moja asubuhi na nyingine jioni hadi pale mmoja ya wateule atafikisha theluthi mbili ya kura zote.
Aidha katika hatua nyingine, makadinali ambao waliondolewa hadhi ya ukadinali na Papa Francis pamoja na kushtakiwa kwa makosa mbalimbali, hawatashiriki zoezi la uchaguzi, licha ya baadhi yao kushinikiza kufanya hivyo akiwemo Angelo Becciu, aliyekutwa na hatia ya matumizi mabaya ya ofisi.