
Maafisa watatu wa ngazi ya juu kutoka bodi ya madini na Petroli nchini Rwanda, wamekamatwa kwa tuhma za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Hatua hii imethibitishwa na Ofisi ya uchunguzi wa makosa ya jinai nchini humo, ambayo imesema pamoja na maafisa hao wa ngazi ya juu, wafanyabiashara wanne, pia wametiwa mbaroni.
Maafisa hao waliokamatwa wametajwa kuwa Augustin Rwomushana, John Kanyangira na Richard Niyongabo, wanazuiwa jinini Kigali, lakini haijafahamika ni lini waliwekwa chini ya ulinzi.
Aidha, haijawekwa wazi iwapo wanahusoshwa na biashara haramu ya madini kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako Rwanda inawashtumuwa kuwaunga mkono waasi wa M23 na kunuifaka na madini ya nchi hiyo.
Hatua hii imekuja baada ya mwezi Machi, Umoja wa Ulaya, kumwekea vikwazo Francis Kamanzi, kiongozi wa bodi ya madini nchini Rwanda, vikwazo kwa kuwaunga mkono waasi wa M23.