
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov siku ya Jumatatu, Aprili 28, ametoa kama sharti la mazungumzo yoyote na Kyiv kutambuliwa na jumuiya ya kimataifa kwa unyakuzi wa Urusi wa Crimea na mikoa mingine ya Ukraine, baada ya Kremlin, kwa upande wake, kusisitiza utayari wake wa majadiliano “bila masharti.” Kutakuwa na makubaliano ya siku tatu kuanzia Mei 8 hadi 10, Vladimir Putin ametangaza.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
“Kutambuliwa kimataifa kwa Crimea, Sevastopol, Jamhuri ya Watu wa Donetsk, Jamhuri ya Watu wa Lugansk, jimbo la Kherson na jimbo la Zaporizhzhia ni sehemu za ardi za Urusi,” Sergei Lavrov amekiambia chombo cha habari cha Brazil O Globo, kulingana na tafsiri ya Kirusi ya mahojiano yake iliyotolewa na wizara yake siku ya Jumatatu, Aprili 28.
Tangu kuagiza jeshi lake kushambulia Ukraine mnamo Februari 24, 2022, Rais wa Urusi Vladimir Putin amedumisha masarti ya juu zaidi ili kufikia mwisho wa mzozo kwa niaba yake. Anadai kujisalimisha kwa Ukraine, kuondolewa kijeshi, kunyimwa uanachama wa NATO, na pia hakikisho la kuweka Peninsula ya Crimea, iliyotwaliwa mwaka 2014, na mikoa minne ya Ukraine ambayo Moscow ilitwaa Septemba 2022.
“Nia” ya Urusi kujadili na Ukraine
Rais wa Urusi anasema kuwa wakati uko upande wake, huku jeshi la Ukraine likipambana katika mstari wa mbele na matakwa yaliyotajwa ya Rais wa Marekani, Donald Trump, ambaye hadi sasa nchi yake ilikuwa muungaji mkono mkuu wa Kyiv, kukomesha uhasama haraka iwezekanavyo, hata ikimaanisha kukubali makubaliano ambayo Waukraine hawaungi mkono.
Katika muktadha huu, na licha ya madai yake yasiyokubalika kwa Kyiv na washirika wake wa Magharibi, Vladimir Putin anahakikisha karibu kila siku kwamba yuko tayari kwa majadiliano ya amani. Siku ya Jumatatu, msemaji wake, Dmitry Peskov, amesisitiza “utayari” wa Moscow kujadili na Kyiv. “Nia ya upande wa Urusi tayari imethibitishwa mara kwa mara, imethibitishwa na rais (Putin), kuanza mchakato wa mazungumzo na Ukraine bila masharti ili kufikia matokeo ya amani,” amesema, kama alivyonukuliwa na shirika la habari l&a serikali ya Urusi, TASS.
Maoni haya yanakuja siku mbili baada ya Donald Trump kutilia shaka nia halisi ya Vladimir Putin: “Labda hataki kusitisha vita na ananifanyia fujo tu,” ameandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social. Hotuba ya Kremlin inatofautiana vikali na matamshi ya kila siku ya Vladimir Putin, akiungwa mkono na Sergei Lavrov siku ya Jumatatu, kulingana na ambayo ni kushindwa kwa Ukraine pekee ndiko kutakubaliwa na Moscow.
Siku ya Jumatatu vikosi vya Urusi vimedai kwamba vilidondosha ndege 115 za Ukraine usiku wa kuamkia Jumatatu katika maeneo kadhaa ya Urusi.