
Baada ya kutengwa katika Mkutano wa Kitaifa wa Mazungumzo ya Syria uliofanyika miezi miwili iliyopita, Utawala unaojiendesha wa Kikurdi uliandaa mkutano wake wa mazungumzo, ambao ulihudhuriwa na vyama vyote vya kisiasa vya Wakurdi vilivyoko katika mikoa ya kaskazini mashariki mwa Syria. Mkutano huu ulifanyika Jumamosi, Aprili 26, katika jiji la Hassaké. Sharti kuu linalojitokeza kutokana na hili ni hakikisho la haki zao za kisheria na kikatiba ndani ya nchi ya kidemokrasia.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu mjini Damascus, Mohamed Errami
Mwishoni mwa mkutano huu, vyama viliwasilisha mlolongo wa madai na masharti ya kuunganishwa kwa mfumo mpya wa utawala wa nchi. Jambo kuu likiwa ni dhamana ya haki zao za kisheria na kikatiba ndani ya nchi ya kidemokrasia na madaraka.
Wanatoa wito wa kuundwa kwa serikali yenye mfumo wa bunge unaozingatia wingi wa kisiasa, uhamishaji wa mamlaka kwa amani, mgawanyo wa mamlaka, na heshima kwa vitambulisho tofauti vya kikabila, kidini na kitamaduni – kwa kuzingatia hasa haki za kitaifa za watu wa Kikurdi.
“Kujenga nchi kwa wote ambapo kila mtu ana nafasi yake”
Katika taarifa yao, Wakurdi pia wametaka katiba ya baadaye ya Syria ihakikishe ahadi ya nchi hiyo kuheshimu mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu, kulinda uhuru na haki za wanawake, na kuhakikisha ushiriki wao kikamilifu katika taasisi zote.
“Tunachotaka sio kuigawanya Syria, bali kujenga nchi ya watu wote ambapo kila mtu ana nafasi yake, lugha yake, utamaduni wake, haki yake,” amesema Mazloum Abdi, kamanda wa Syrian Democratic Forces (SDF) katika ufunguzi wa mkutano huo.
Vyama vya Wakurdi pia vimeangazia suala la lugha, vikitaka kutambuliwa kikatiba kwa lugha ya Kikurdi kama lugha rasmi pamoja na Kiarabu, na kwamba jina la serikali, bendera yake na wimbo wake wa kitaifa zinaonyesha tofauti za kikabila na kitamaduni za jamii ya Syria.
Tamko la mwisho kwa hivyo linajumuisha wito wa wazi wa marekebisho ya Katiba, toleo la awali ambalo Rais wa Syria Ahmed Al-sharaa aliidhinisha katikati ya mwezi Machi.