Jenerali auawa karibu na Moscow: Idara ya ujasusi ya Urusi yatangaza kukamatwa kwa mshukiwa

FSB imetangaza katika taarifa Jumamosi, Aprili 26, kukamatwa kwa “afisa wa idara maalum ya Ukraine Ignat Kuzin, aliyezaliwa mwaka wa 1983 na anayeishi Ukraine.” Anatuhumiwa kwa kifo cha Luteni Jenerali Yaroslav Mosklyk, ambaye aliuawa siku moja kabla katika mlipuko wa gari huko Balashikha, mkoa wa Moscow.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Mshukiwa huyo kwa sasa anahojiwa na wachunguzi, Kamati ya Uchunguzi ya Urusi imesema. Anashutumiwa kwa kutega, kwa manufaa ya Ukraine, bomu lililolipua gari la afisa huyo wa ngazi ya juu katika jeshi la Urusi siku ya Ijumaa hii.

Idara ya usalama ya Urusi (FSB) imetangaza siku ya Jumamosi kukamatwa kwa mtu anayefanya kazi nchini Ukraine, anayeshukiwa kumuua jenerali wa Urusi katika mlipuko wa gari karibu na Moscow.

Urusi ilikuwa tayari imeishutumu Kyiv kwa kuhusika na mlipuko uliomuua Jenerali wa Urusi Yaroslav Moskalik, naibu mkuu wa siku ya Ijumaa. “Afisa wa idara maalum ya Ukrain Ignat Kuzin, aliyezaliwa 1983 na anayeishi Ukraine, ambaye alitega vilipuzi kwenye gari aina ya Volkswagen Golf huko Balashikha, mkoa wa Moscow, na kumuua Luteni Jenerali Yaroslav Moskalik, amekamatwa,” FSB imesema katika taarifa.

Bomu llililotengenezwa kienyeji

Kulingana na FSB, mtu huyo alikuwa alitega bomu lililotengenezwa kienyeji kwenye gari la jenerali huyo, ambalo alilichukua kwenye maficho ya idara maalumu ya Ukraine katika mkoa wa Moscow. Bomu hilo lililipuliwa kidhibitimbali (rimoti) kutoka Ukraine, inadai FSB.

Mshukiwa, ambaye anakabiliwa na kifungo cha maisha ikiwa atapatikana na hatia ya “ugaidi,” kwa sasa anahojiwa na wachunguzi, kulingana na Kamati ya Uchunguzi ya Urusi, chombo kinachohusika na kesi nyeti zaidi. Ukraine haijazungumza lolote kuhusu shambulio hilo ambalo ni sawa na mashambulizi mengine yaliyotekelezwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita dhidi ya maafisa wa ngazi za juu wa jeshi la Urusi na wafuasi wenye ushawishi mkubwa wa Kremlin.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *