Mahmoud Abbas amteua mshauri wa karibu, Hussein al-Sheikh, kama makamu mwenyekiti wa PLO

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amemteua mshauri wa karibu, Hussein al-Sheikh, kwa nafasi mpya iliyoundwa ya makamu wa rais wa Chama cha Ukombozi wa Palestina (PLO) Jumamosi, Aprili 26, na kumfanya kuwa mrithi wake mtarajiwa.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

“Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amemteua Hussein al-Sheikh kama amiri wa pili katika uongozi wa Chama cha Ukombozi wa Palestina,” Wasel Abu Youssef, mjumbe wa kamati kuu ya PLO, ameliambia shirika lahabari la AFP.

Nafasi hii ilianzishwa rasmi siku ya Alhamisi, kwa mpango wa Mahmoud Abbas mwenyewe, wakati wa kongamano huko Ramallah, katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, kwani jumuiya ya kimataifa kwa muda mrefu imekuwa ikiitaka PLO kufanya mageuzi.

Hussein al-Sheikh, 64, ni mkongwe wa chama cha Fatah cha Mahmoud Abbas na anachukuliwa kuwa karibu naye. Kwa mujibu wa Aref Jaffal, mkurugenzi wa Kituo cha Al-Marsad cha Ufuatiliaji wa Uchaguzi, kuundwa kwa nafasi ya makamu mwenyekiti wa PLO, chama kilichopewa mamlaka ya kujadili na kuhitimisha mikataba ya kimataifa kwa niaba ya watu wa Palestina, kunalenga “kutayarisha urithi wa Abbas.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *