
Kufuatia shambulio la kigaidi lililolenga watalii huko Kashmir ya India, mvutano kati ya India na Pakistani umefikia kiwango ambacho hakijaonekana katika robo karne. Kufuatia msururu wa hatua za ulipizaji zilizochukuliwa na India dhidi yake, Pakistan siku ya Alhamisi ilipiga marufuku safari za ndege za abiria za India kutoka kwenye anga yake, ikafunga mpaka mkuu kati ya nchi hizo mbili na kutaka kuondoka kwa makumi ya wanadiplomasia wa India. Je, India na Pakistan ziko ukingoni mwa vita?
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu katika Islamabad, Sonia Ghezali
Mvutano kati ya India na Pakistani uliongezeka Alhamisi jioni na vikosi kutoka nchi zote mbili vilirushiana risase kwenye Mstari wa Udhibiti unaotenganisha nchi hizo mbili. Hali hii ni mbali na ya kutisha, hata hivyo, kulingana na Zeeshan Salahuddin, mchambuzi wa kisiasa katika kituo cha utafiti cha Tabadlab huko Islamabad.
“Kuongeeka kwa uhasama katika Bonde la Leeppa si jambo la kawaida. Tusisahau kwamba Pakistani na India zimepigana vita vingi na kati ya vita hivi, hasa katika Mstari wa Udhibiti, mapigano yametokea mara kwa mara,” anasema.
Hii ilikuwa kesi haswa mnamo 2019 baada ya shambulio la kujitoa mhanga huko Kashmir ya India lililodaiwa na kundi lenye silaha. “Wakurugenzi wakuu wa oparesheni za kijeshi wa pande zote mbili wanawasiliana mara kwa mara ili kujaribu kupunguza baadhi ya matukio haya. Lakini hii ni sehemu tofauti sana ya dunia kutokana na kuongezeka na mapigano kwenye mstari wa Udhibiti au kile kinachotokea kati ya Pakistani na India. Katika hali nyingi za kawaida, hatimaye mambo hufanikiwa. Umiliki wa silaha za nyuklia kwa kila moja ya nchi hizo mbili umekuwa karibu kila mara kuwa kipengele muhimu cha kumalizika kwa vita. “Kwa hivyo ninatarajia kuwa hali hiyo huenda ikajirusi wakati huu,” mchambuzi pia anabainisha.
Pakistani bado inaonyesha uimara wake. Jeshi limeripotiwa kupata amri ya kujiandaa na hali mbaya zaidi. Vikosi vya usalama viko macho, chanzo kilicho karibu na jeshi kimetuambia. Wanajeshi pia wameripotiwa siku ya Ijumaa katika pande zote za mpaka wa Kashmir, na matuiko kadhaa ya urushianaji risai yaliripotiwa kwenye mpaka. Hakuna vifo vya raia vilivyoripotiwa.
Vikosi vya India na Pakistani pia vilifyatuliana risasi usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi kwenye Mstari wa Udhibiti (LoC), mpaka wa ukweli kati ya India na Pakistan huko Kashmir. Kulingana na shirika la habari la AFP, jeshi la India limesema kuwa ngome zake za wanajeshi zilifyatua risasi nyingi “kando ya Mstari wa Udhibiti huko Kashmir” siku ya Ijumaa usiku.
“Uchunguzi usiogemea upande wowote”
New Delhi inamtuhumu jirani yake kuhusishwa na shambulizi lililoua raia 26 katika eneo la Pahalgam, huko Kashmir ya India. Jeshi la India siku ya Ijumaa liliharibu nyumba mbili kwa vilipuzi ambavyo vilisemekana kuwa vya familia za wahusika wa shambulio hilo.
Kwa upande wake, wakati wa sherehe za kijeshi, Waziri Mkuu wa Pakistani Shehbaz Sharif alitangaza kuunga mkono “uchunguzi usioegemea upande wowote” wa shambulio la Kashmir ambalo India inalaumu Pakistani. Hizi ni “tuhuma zisizo na msingi,” alisema, akiongeza kuwa “mauaji haya ya hivi majuzi ni mfano mwingine wa lawama hizi za kudumu ambazo lazima zikome.”