
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio anatarajiwa kushuhudia utiaji saini wa makubaliano kati ya DRC na Rwanda, baada ya serikali ya Kinshasa na waasi wa M 23 kukubaliana kuhakikisha vita vinasitishwa.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani imesema, Waziri Rubio atatia saini mkataba unaonesha utaratibu wa kusuluhisha mvutano kati ya nchi hizo mbili ambazo uhusiano wao wa kidiplomasia umeyumba, kati yake na mwenzake wa Rwanda Olivier Nduhungirehe na Therese Kayikwamba Wagner wa DRC.
Hata hivyo, maelezo ya kina kuhusu kitakachosainiwa, hakijawekewa wazi, lakini inakuja siku moja tu baada ya waasi wa M 23 na wawakilishi wa serikali ya Kinshasa, waliokuwa wanakutana jijini Doha kukubaliana kuendelea kushirikiana ili kuleta amani ya kudumu Mashariki mwa DRC.
Haya yanajiri pia wiki moja baada ya Massad Boulos, mjumbe maalum wa rais Donald Trump kufanya ziara ya kikanda na kuiambia Rwanda kuondoa wanajeshi wake Mashariki mwa DRC na kuacha kuwaunga mkono waasi wa M23, madai ambayo Rwanda imekuwa ikikanusha.
Serikali ya rais Felix Thisekedi, imeomba msaada wa Marekani kusaidia kurejesha amani Mashariki mwa DRC na kuingia kwenye mkataba kuhusu biashara ya madini.