KESI YA LISSU UPDATES: Mtandao changamoto,hakimu aahirisha kwa muda

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeahirisha kwa muda kesi ya kusambaza taarifa za uongo katika mtandao wa Youtube inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu.

Uamuzi huo umetolewa leo, April 24, 2025 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Geoffrey Mhini wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa njia ya video, ili mshtakiwa asomewa hoja za awali.

Hakimu Mhini amesema kutokana na mtandao kusumbua, anaahirisha kwa muda na kama utakuwa bado kuna changamoto atatoa uamuzi.

Hata hivyo, ukumbi huo wa video conference uliopo katika Mahakama hiyo, umejaa hali iliyosababisha baadhi ya watu kuzuiwa kuingia.

Endelea kutembelea mitandao ya kijamii ya Mwananchi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *