DRC: M23 na Kinshasa zakubaliana kuendeleza mazungumzo ya kusitisha vita

Kuna Maendeleo chanya katika mazungumzo kati ya AFC/M23 na wajumbe kutoka ofisi ya rais wa Kongo. Kwa mara ya kwanza pande hizo mbili zimewasiliana rasmi kuhusu mazungumzo hayo yaliyofanyika mjini Doha. Jana, katika taarifa ya pamoja, wawakilishi wa DRC na wale wa AFC/M23 walitangaza kwamba wamekubali “kufanyia kazi kuhitimisha mapatano” kwa nia ya kusitisha mapigano kikamilifu.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Haya bado sio makubaliano ya kusitisha mapigano. Wala sio mapatano.Katika hatua hii, ni tamko tu la nia, taarifa ambayo pande zote mbili zinathibitisha makubaliano yao ya kufanya kazi pamoja kuelekea makubaliano.

Kama ilivyoripoti hapo awali na RFI, maandishi haya yalikuwa tayari tangu Aprili 17. Iliandaliwa siku nne baada ya kumalizika kwa majadiliano ya moja kwa moja kati ya wajumbe wa Kinshasa na wale wa AFC/M23. Kilichokosekana ni idhini rasmi ya Félix Tshisekedi.

RFI Data / Qatar : via REUTERS - Qatar's Ministry of Foreign Affa
Rais wa DRC na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame walipokutana nchini Qatar. © via REUTERS – Qatar MAE / archive RFI

Sasa imefanyika kama ilivyosubiriwa baada  ya hapo  jana usiku, rais wa Kongo kukubali, ambapo hati ilichapishwa mara moja, kwa pamoja na pande zote mbili.

Hatua inayofuata sasa ni wakati wa kuheshimu ahadi zilizotolewa, kabla ya kuanza kwa mazungumzo ya kweli na muhimu. Miongoni mwa ahadi hizi ni kutotumia kauli za vitisho na kuonyesha nia ya dhati ya kuunda hali ya hewa inayofaa kwa mazungumzo.

Wapiganaji wa Wazalendo na wanajeshi wa serikali ya DRC wamekuwa wakipambana na makundi ya waasi mashariki ya DRC.
Wapiganaji wa Wazalendo na wanajeshi wa serikali ya DRC wamekuwa wakipambana na makundi ya waasi mashariki ya DRC. REUTERS – Arlette Bashizi

Mazungumzo yanayotarajiwa lazima yalenge, kulingana na pande zote mbili, juu ya sababu kuu za mzozo na njia madhubuti za kurejesha amani katika maeneo ya mashariki.

Tangazo hili pia linakuja siku moja baada ya mkutano kati ya Waziri wa Nchi wa Qatar Mohammed Al-Khulaifi, anayehusika na suala hilo, na Massad Boulos, Mshauri Mkuu mpya wa White House kwa Afrika. Mkutano huu ni sehemu ya juhudi za pamoja za kuondoa uhasama wa kudumu katika kanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *