Burundi: Rais wa Tume ya kutetea haki za binadamu atoroka nchi

Rais wa Tume huru ya kutetea haki wa binadamu nchini Burundi, CNIDH Sixte Vigny NIMURABA, amelazimika kukimbia nchi, baada ya kuripotiwa kuingia kwenye matatizo na watu wenye mamlaka serikalini.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Matangazo ya kibiashara

Hatua ya NIMURABA, kuondoka nchini humo, inaelezwa ni kutokana na ripoti ambayo tume yake, ilitoa mwaka 2024 kuelezea hali ya haki za binadamu nchini Burundi.

Spika wa bunge Gélase-Daniel Ndabirabe, anatuhumiwa kuwa nyuma ya masaibu yaliyomkuta NIMURABA, na kuamua kukimbia nchi baada ya kushtumiwa kuchafua sifa ya nchi.

Mkuu huyo wa Tume ya Haki za binadamu, ameshtumiwa kwa kuhusika na kupotea kwa Euro Laki nne, kwa kipindi cha miaka miwili, baada ya Makamishena watatu kujitokeza kulalamikia kupotea kwa fedha hizo.

Tangu katikati ya mwezi huu, Spika wa bunge ameripotiwa kushinikiza mabadiliko kwenye Tume hiyo, na kupelekea msako nyumbani kwa NIMURABA, ambaye alilazimika kukimbia nchi hiyo pamoja na familia yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *