Vita vya kibiashara: Beijing iko wazi kwa majadiliano na Washington

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza siku ya Jumanne, Aprili 22, kwamba anataka kuhitimisha makubaliano “kwa kiasi kikubwa” kupunguza ushuru wa forodha unaolenga China. Beijing inasema iko wazi kwa majadiliano na Washington. Tangazo lililopokelewa vyema na masoko.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Washington “bado haijafanya mazungumzo na Beijing kuhusu ushuru,” Waziri wa Fedha wa Marekani Scott Bessent amesema siku ya Jumatano Aprili 23 wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Marekani. “Nadhani pande zote mbili zinangoja kuzungumza,” Bessent amesema, akiongeza kuwa Trump hakutoa punguzo lolote la ushuru wa upande mmoja, licha ya ripoti katika vyombo vya habari vya Marekani juu ya kupunguza uwezekano wa ushuru kwa bidhaa za China. “Ningeshangaa ikiwa mazungumzo haya yalifanyika,” Waziri wa Fedha ameongeza.

Kwa mujibu wa jarida la Wall Street Journal, ambalo linanukuu vyanzo vilivyo karibu na suala hilo, utawala wa Trump unafikiria kupunguza ushuru wa Marekani kwa bidhaa kutoka China.

Kando ya sherehe katika Ikulu ya White House, rais wa Marekani alikiri kwa vyombo vya habari kwamba 145% ya malipo ya ziada, ambayo yeye mwenyewe aliweka kwa Beijing, yalikuwa “ya juu sana” na kwamba “yatapungua kwa kiasi kikubwa.” “malipo hayataendelea kuwa karibu na takwimu hiyo kwa hali yoyote,” alisema, na kuongeza, hata hivyo, kwamba “hatutarudi kwa sifuri.” “Tutatafanya mambo ya kuwafurahisha ndugu zetu, na wao vile vile vile, na tutaona kitakachotokea,” Trump aliongeza. “Tutaweka masharti ya makubaliano na yatakuwa makubaliano ya haki. “Nadhani ni mchakato ambao utaenda haraka sana,” alitabiri.

“Ikiwa itabidi tupambane, tutakwenda hadi mwisho, lakini milango ya mazungumzo bado iko wazi,” Guo Jiakun, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, amesema katika mkutano wa kila siku na wanahabari siku ya Jumatano.

Uhakikisho kwa masoko

Matumaini ya uwezekano wa kusitishwa kwa uhasama kulifanya masoko ya fedha kuimarika siku ya Jumatano, haswa kama vile Donald Trump pia alitangaza siku ya Jumanne kwamba “hakuwa na nia” ya kumfukuza mwenyekiti wa Hifadhi ya Shirikisho la Marekai (Fed), baada ya ukosoaji wake mbaya dhidi ya Jerome Powell kupelekea soko la fedha kuyumba.

Katika Asia, masoko ya hisa yalikuwa yakipanda tena, kutoka Tokyo hadi Hong Kong, na dola ilikuwa ikipata nguvu tena. Soko la Hisa la New York limefunguliwa kwa kasi zaidi, likiwa limehakikishiwa na matumaini ya uwezekano wa kusitishwa kwa uhasama na kwa matamshi ya maridhiano ya Donald Trump kuhusu Fed.

China ilitoa wito kwa Uingereza na Umoja wa Ulaya siku ya Jumanne kutetea biashara ya kimataifa katika kukabiliana na mashambulizi ya Marekani. “Katika mazingira ya sasa ya kuenea kwa uonevu wa upande mmoja, China na Uingereza zina jukumu la kulinda utaratibu wa kibiashara wa pande nyingi,” Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi alimwambia mwenzake wa Uingereza David Lammy katika simu, kulingana na taarifa kutoka wizara yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *