Wakati huu Vatican ikiwa imeanza maandalizi ya mazishi ya aliyekuwa kiongozi wake Papa Francis ambaye atazikwa wikendi hii, tayari mjadala umeanza kuhusu makadinali wanaoweza kumrithi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Wa kwanza ni Kadinali Peter Erdo, miaka 72 ni askofu wa Budapest ambaye kwa zaidi ya mara mbili alichaguliwa kuongoza baraza la maaskofu la Ulaya kati ya mwaka 2005 na 2011, akiungwa mkono wenzake wa Ulaya na wale kutoka Afrika.

Mwingine ni Reinhard Marx, miaka 71 ni askofu wa dayosisi ya Munich, alichaguliwa kuwa mshauri mwandamizi wa Papa mwaka 2023 kabla ya baadae kuteuliwa kusimamia masuala ya fedha ya Vatican.

Kadinali Marc Quellet mwenye umri wa miaka 80 raia wa Canada ni mtu mwingine anayepewa nafasi na kwa miongo kadhaa alikuwa kiongozi la jopo la kuchuja makadinali wanaoteuliwa na papa tangu kipindi cha Papa benedict wa 16.

Kadinali Pietro Parolin mwenye umri wa miaka 70 ni muitaliano ambaye amekuwa katibu wa papa tangu mwaka 2014, akitajwa kama mmoja ya watu walio vinara kupewa nafasi hiyo.

Kadinali Robert Sarah wa Guinea, ni mtu mwingine anayepewa nafasi ingawa hakuwa na uhusiano mzuri na Papa kutokana na kuwa na msimamo mkali kuhusu tamaduni za kanisa tofauti na papa francis alivyokuwa.
Kadinali Luis Tagle wa Ufilipino, yeye ana umri wa mliaka 67 na huenda akawa Papa wa kwanza kutoka ukanda wa Asia ikiwa atachaguliwa, na aliteuliwa na Papa kuongoza kitengo cha uinjilisti cha Vatican.

Wemo pia kadinali Matteo Zuppi wa Bolongya mwenye umri wa miaka 69, Robert Prevost raia wa Marekani mwenye miaka 69, kadinali Christoph Schoenborn raia wa Austria mwenye umri wa miaka 80.