
Rais wa Kenya William Ruto amewasili Beijing siku ya Jumanne jioni, Aprili 22, kwa ziara ya kiserikali itakayoendelea hadi Aprili 26, kwa mwaliko wa mwenzake wa China. Moja ya malengo ya Nairobi ni kufungua fursa mpya katika biashara, uwekezaji na miundombinu. Mazungumzo ya nchi mbili na Xi Jinping ni ajenda katikati ya vita vya kibiashara kati ya China na Marekani.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, Albane Thirouard
“Tunatafuta kuimarisha na kupanua uhusiano wa kihistoria, kiuchumi na kiutamaduni kati ya Kenya na China.” Haya ndiyo aliyoandika rais William Ruto kwenye mtandao wa kijalii wa X alipowasili Beijing.
Hatua yake ni sehemu ya mkakati wa mseto kwa upande wa Nairobi, anabainisha mwanauchumi XN Iraki, hasa kwa fursa mpya za soko. Haya yanajiri huku bidhaa za Kenya zikiathiriwa na tozo ya 10% ya forodha iliyowekwa na Donald Trump.
Hivi sasa, uwiano wa kibiashara kati ya Beijing na Nairobi unaipendelea China. Kenya inataka kuongeza mauzo yake ya nje, hasa ya bidhaa za kilimo kama vile chai. Nairobi pia inataka kuwa na wafadhili wangi kwa miradi ya maendeleo.
Kenya inajitahidi kukabiliana na mzigo wake wa madeni na kwa hivyo inatumai kujadili ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi na Beijing. Majadiliano hayo yatalenga upanuzi wa njia ya reli kutoka Naivasha, kaskazini-magharibi mwa Nairobi, hadi Malaba kwenye mpaka na Uganda, na barabara kuu inayopendekezwa kuunganisha Nairobi hadi Mau Summit, kaskazini mwa nchi.
Nairobi na Beijing zinatarajiwa kutia saini mikataba kadhaa katika sekta mbalimbali: biashara, miundombinu, elimu na uhamisho wa teknolojia.