Tamasha la “Congo Solidarity” lafanyika jijini Paris

Hatimaye Tamasha la “Congo Solidarity” limefanyika Jumanne Aprili 22, katika Ukumbi wa Accor Arena, mjini Paris Ufaransa (baada ya kuahirishwa kwa sababu tarehe ya awali ya Aprili 7 ililingana na kuanza kwa kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya Watutsi nchini Rwanda, ambayo yalizua utata)

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Tamasha hili la kipekee lililenga kuchangisha fedha “kusaidia watoto wahanga wa mzozo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo”... Tukio hili liliwaleta pamoja karibu watu 11,000 na takriban wasanii thelathini – wakiwemo magwiji Fally Ipupa, Youssoupha, Gims, Sidiki Diabate na Dadju.

Baadhi ya wanachama wa mashrika ya kimataifa walihamasishwa kabla ya tamasha hili ambapo bendera za DRC zilisambazwa kwa watazamaji walioshuhudia tamasha hilo huku wakipeperusha bendera hizo.

Manusura wa mauaji mashariki mwa DRC walitoa ushuhuda kwa madhila waliokutana nayo huko mashariki mwa DRC. Awali tamasha hili lilipangwa kufanyika April 7, tarehe ambayo nchi ya Rwanda huanda maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari, na kuzua mtafaruku mkubwa kabla ya kuahirishwa.

Waandalizi wa tamasha hili la Solidarité Congo walitangaza onyesho kiingilio ilikuwa ni bure, na mapato yakienda kwa  shirika la Give Back Solidarity la muimbaji Dadju’s. Shirika hili lina jukumu la kusambaza mapato hayo kwa walengwa nchini DRC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *