Shambulio dhidi ya watalii huko Kashmir India: angalau 24 wafariki

Watu wenye silaha wamefyatulia risasi kundi la watalii huko Kashmir nchini India mnamo Jumanne, Aprili 22, na kuua takriban watu 24, afisa mkuu wa polisi wa India amesema. Hakuna idadi rasmi ya vifo ambayo imetangazwa, lakini mamlaka imetaja kuwa ni shambulio baya zaidi kwa raia katika miaka.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

“Ninalaani vikali shambulio hili dhidi ya watalii huko Pahalgam (…),” amesema Mehbooba Mufti, diwani wa zamani wa eneo hilo na kiongozi wa chama cha upinzani.

Mkuu wa serikali za mitaa Omar Abdullah amesema idadi ya waliouawa “inaendelea kuthibitishwa,” lakini akasisitiza kwamba “shambulio hilo ni kubwa zaidi kuliko chochote ambacho tumeona kikilenga raia katika miaka ya hivi karibuni.” “Shambulio hili dhidi ya watu wanaotutembelea ni chukizo,” amesema katika taarifa.

“Magaidi hawa wamelenga watalii wasio na hatia, wasio na silaha ambao walikuja kutembelea Kashmir,” Ravinder Raina, mwanachama wa BJP, chaa cha Waziri Mkuu Narendra Modi, ameviambia vyombo vya habari vya India. “Baadhi ya watalii wameliojeruhiwa wamelazwa katika hospitali ya eneo hilo,” ameongeza.

Hadi sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo.

Shambulizi hilo lilitokea katika eneo la Pahalgam, kivutio maarufu cha watalii takriban kilomita 90 kutoka mji mkuu wa Srinagar. India ina takriban wanajeshi 500,000 waliotumwa kabisa katika eneo hilo, ingawa mapigano yamepungua tangu serikali ya Narendra Modi ilipobatilisha uhuru mdogo wa Kashmir mnamo 2019.

Tangu wakati huo, mamlaka ya India imetangaza eneo hili la milima kama kivutio cha watalii, kwa kuteleza kwenye theluji wakati wa miezi ya msimu wa baridi na kama njia ya kuepuka joto kali la kiangazi katika maeneo mengine ya India. Takriban watalii milioni 3.5 walitembelea Kashmir mnamo mwaka 2024, wengi wao wakiwa watalii wa India, kulingana na takwimu rasmi.

Mnamo mwaka 2023, India iliandaa mkutano wa kitalii wa G20 huko Srinagar chini ya ulinzi mkali ili kuonyesha kuwa utulivu ulikuwa umerejea baada ya ukandamizaji mkubwa uliofuata kufutwa kwa New Delhi kwa uhuru mdogo wa mkoa mnamo mwaka 2019.

Vivutio vingi vya watalii vinaendelea kutengenezwa, vikiwemo vingine vilivyo karibu na mpaka wa kijeshi unaogawanya Kashmir kati ya India na Pakistan.

India mara kwa mara inaishutumu Pakistan kwa kuunga mkono wanamgambo Kwa upande wake, Islamabad inakanusha shtaka hili, ikithibitisha tu uungaji mkono wake wa kujitawala kwa Kashmir.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *