Mauritius: Rais wa Ufaransa ‘aahirisha ziara ya kiserikali ili kuhudhuria mazishi ya Papa’

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye ameanza ziara ya siku tano katika Bahari ya Hindi huko Mayotte mnamo Aprili 21, “amelazimika kuahirisha ziara yake rasmiya kiserikali [tarehe 25 Aprili] nchini Mauritius ili kuhudhuria mazishi ya Papa” ambayo yatafanyika Aprili 26, Ikulu ya Élysée imetangaza Aprili 22, 2025.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa atakutana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mauritius Ram Navin. Mauritius pembezoni mwa mkutano wa Kamisheni ya Bahari ya Hindi (IOC) ili kuhakiki vipengele mbalimbali vya uhusiano baina ya nchi hizo mbili,” taarifa hiyo inaongeza.

Kulingana na Vatican, kiongozi wa Kanisa Katoliki atazikwa siku ya Jumamosi Aprili 26.

Papa Francis, aliyefariki siku ya Jumatatu akiwa na umri wa miaka 88, Vatican imesema kifo chake kilisababishwa na kiharusi na matatizo ya moyo.

Watu wanatarajiwa kuanza kumuaga siku ya Jumatano. Kote duniani, baada ya kifo chake, Wakiristo na wasio Wakiristo wamekuwa wakifurika katika Makanisani, kuhudhuria misa ya kumkumbuka kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki.

Akiwa hai, Papa Francis aliomba kuzikwa katika Kanisa la Mtakatifu Maria Major Basilica, eneo ambalo viongozi wa Kanisa hilo huzikwa. Watu wanatarajiwa kuanza kumuaga siku ya Jumatano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *