
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linasikitishwa kwamba litalazimika kusitisha misaada nchini Ethiopia mwezi Mei kwa wanawake na watoto 650,000 wenye utapiamlo kutokana na ukosefu wa fedha.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Bila msaada wa dharura, watu milioni 3.6 hawataweza tena kupata msaada wa chakula “katika wiki zijazo,” shirika la Umoja wa Mataifa pia limeonya katika taarifa yake.
WFP, “italazimika kusitisha kuwahudumia wanawake na watoto 650,000 wenye utapiamlo mwezi Mei,” imepanga kutoa msaada wa lishe ya kuokoa maisha kwa akina mama na watoto milioni 2 mwaka 2025.
Mbali na uamuzi wa Donald Trump wa kusitisha programu za misaada chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) baada ya kurejea Ikulu ya White House, nchi kadhaa za Magharibi zimepunguza matumizi yao katika suala hili. Licha ya mahitaji yanayoongezeka, WFP “inatarajia kupokea zaidi ya nusu ya ufadhili wa mwaka jana kwa shughuli zake nchini Ethiopia.” Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linakabiliwa na “pengo la ufadhili la dola milioni 222 kati ya mwezi Aprili na Septemba 2025,” limeonya.