Vatican imesema mazishi ya kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis yatafanyika siku ya Jumamosi.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Baadhi ya viongozi ambao wamethibitisha kuhudhuria mazishi yake ni pamoja Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky.
Papa Francis, aliyefariki siku ya Jumatatu akiwa na umri wa miaka 88, Vatican imesema kifo chake kilisababishwa na kiharusi na matatizo ya moyo.
Uongozi wa Vatican ulithibitisha kifo chake, na kusema Papa Francis alifariki dunia saa moja na dakika 35 asubuhi, siku ya Jumatatu, wiki kadhaa baada ya kuruhusiwa hospitalini, alikolazwa kwa zaidi ya mwezi mmoja, baada ya kusumbuliwa na nimonia.
Mwili wa Papa Francis umepelekwa Kanisani, huku maombolezo yakiendelea.
Akiwa hai, Papa Francis aliomba kuzikwa katika Kanisa la Mtakatifu Maria Major Basilica na sio Mtakatifu Petro, eneo ambalo viongozi wa Kanisa hilo huzikwa. Watu wanatarajiwa kuanza kumuaga siku ya Jumatano.
Kote duniani, baada ya kifo chake, Wakiristo na wasio Wakiristo wamekuwa wakifurika katika Makanisani, kuhudhuria misa ya kumkumbuka kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki.