Ripota wa UN amkemea balozi wa US kwa kuunga mkono ‘jinai ya kivita’ ya Israel ya kuizuilia misaada Ghaza

Ripota maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binadamu katika ardhi za Palestina amemuonya balozi mpya wa Marekani katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu zilizopachikwa jina bandia la Israel kwamba kuzuia misaada ya kibinadamu isiingizwe katika Ukanda wa Ghaza uliowekewa mzingiro ni uhalifu wa kivita.