
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro amemwita mwenzake wa Salvador, Nayib Bukele, “mkiukaji wa haki za binadamu” baada ya kujitolea kubadilishana Wavenezuela 252 waliozuiliwa nchini mwake baada ya kufukuzwa na Marekani kwa “wafungwa wa kisiasa” wanaoshikiliwa nchini Venezuela.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
“Ni mkiukaji wa utaratibu na mfululizo wa haki za binadamu tangutoka El Salvador dhidi ya Wavenezuela,” Nicolas Maduro ametangaza Jumatatu, Aprili 21, wakati wa kipindi chake cha televisheni cha kila wiki.
“Kutokana na ukiukwaji kamili wa haki za binadamu, ninamwambia: ‘Bwana Bukele, zingatia sheria (…) toa uthibitisho wa maisha kwa vijana wote waliotekwa nyara.’ Eleza mahali ambapo kuna mchakato wa kisheria, kwa sababu gani, ni uhalifu gani wamefanya, kuruhusu upatikanaji wa wakili (…) Kataa njia ya kutoweka kwa kulazimishwa, na mapema au baadaye, waachilie bila masharti,” ameongeza.
“Uhuru usio na masharti kwa vijana waliotekwa nyara huko El Salvador,” amesema, akibaini kwamba kufungwa kwa Wavenezuela huko El Salvador ni “uhalifu mkubwa dhidi ya ubinadamu.”
Mapema siku hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Venezuela Tarek William Saab pia alidai “uhuru usio na masharti” kwa wahamiaji, akitoa wito kwa mamlaka ya El Salvador kujibu “mawasiliano” na “rufani” za kisheria zilizotumwa na Caracas.
Ameongeza kuwa “mtu hawezi kulinganisha” Wavenezuela waliozuiliwa huko El Salvador “bila kufuata utaratibu” na “wale waliokamatwa (nchini Venezuela) kwa jaribio la kumuua rais (…) wakitaka kulipua kambi, au utekaji nyara.”
Serikali ya Venezuela mara kwa mara inashutumu njama za kweli au za kufikirika.
“Mkataba wa kibinadamu”
Siku ya Jumapili, Nayib Bukele, mshirika mkuu wa Rais wa Marekani Donald Trump, alipendekeza kwa Caracas “makubaliano ya kibinadamu ambayo yanatoa fursa ya kurejeshwa nyumbani kwa 100% ya Wavenezuela 252 (…) ili kubadilishana na kuachiliwa na kukabidhi idadi sawa (252) ya maelfu ya wafungwa wa kisiasa inayowashikilia.”
Katika muda wa mwezi mmoja tu, amewapokea na kuwafungia katika gereza lenye ulinzi mkali wahamiaji 288 waliofukuzwa kutoka Marekani, wakiwemo Wavenezuela 252, ambao wengi wao wanatuhumiwa kuwa wa genge la Tren de Aragua, kundi la uhalifu wa kimataifa lililotangazwa kundi la “kigaidi” na Washington.
Siku ya Jumamosi, Rais wa Colombia Gustavo Petro alitoa wito kwa mwenzake wa El kuwakabidhi raia wa Colombia waliofukuzwa kutoka Marekani na kuzuiliwa katika kituo kimoja.
Ili kuwafukuza wahamiaji hawa hadi El Salvador, Bw. Trump alipendekeza “Alien Enemies Act” ya mwaka 1798, ambayo hapo awali ilikuwa ikitumika tu wakati wa vita.
Siku ya Jumapili Donald Trump aliwakashifu majaji waliopinga sera hiyo, siku moja baada ya msukosuko mkubwa kutoka kwa Mahakama ya Juu.