
Uongozi wa kijeshi nchini Burkina Faso unasema, umefanikiwa kuzuia jaribio la mapinduzi, mpango ambao jeshi linasema limeandaliwa katika nchi jirani ya Cote Dvoire.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Jeshi nchini Burkina Faso linaloongoza nchi hiyo tangu 2022, linasema, jaribio hio, lilenga kuleta vurugu katika nchi yake.
Tangu alipochukua madaraka, kiongozi wa kijeshi Captain, Ibrahim Traore, amekuwa akiilaumu Cote Dvoire kwa kuwapa hifadhi maadui wa serikali ya kijeshi.
Waziri wa usalama Mahamadou Sana, amesema taarifa za kiiteljensia zinaonesha mpango unaoadaliwa kuleta vurugu nchini humo na wanajeshi, aliosema wanaifadhiwa na maadui wa nchi ya Burkina Faso.
Aidha, Waziri huyo amesema kulikuwa na mpango wa kuvamia maakazi ya kiongozi wa nchi hiyo Aprili tarehe 16, lakini ukazuiwa, waliokuwa maafisa wa jeshi Meja Joanny Compaore na Luteni Abdramane Barry wakitajwa kuhusika.
Wiki iliyopita, maafisa kadhaa wajeshi walikamatwa, kwa madai ya kuwa na mpango wa kusababisha vuruu nchini Burkina Faso, ambayo tangu mwaka 2015 imekuwa ikisumbuliwa na makundi ya kijihadi.