
Emmanuel Macron anasafiri hadi Mayotte asubuhi ya leo, Jumatatu, Aprili 21, kituo cha kwanza katika ziara ya siku tano katika Bahari ya Hindi, ambayo itampeleka Rais wa Ufaransa hadi Réunion, Madagascar, na Mauritius. Mkuu wa nchi alizuru Mayotte mnamo mwezi Desemba baada ya Kimbunga Chido na kuahidi kurejea.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Ahadi iliyotolewa sasa inatekelezwa. rais Wa Ufaransa Emmanuel Macron anarejea Mayotte. Alizuru Mayotte mara moja wakati Kimbunga Chido kilipoharibu visiwa hivyo ili kujionea ukubwa wa uharibifu huo. Hakuna umeme tena, hakuna maji, hakuna shule tena, raia wako katika hali ngumu … hali ni mbaya zaidi.
Emmanuel Macron aliwaahidi raia wa Mayotte kujenga upya haraka kwa kutumia njia kama ile iliyotumiwa kwa ujenzi wa Kanisa Kuu la Notre-Dame huko Paris. Ahadi hizi hazikutuliza hasira za baadhi ya wakazi waliomchukulia vibaya Emmanuel Macron, wakimtuhumu kuitelekeza Mayotte.
Moja ya changamoto leo ni kuonyesha kwamba mambo yanasonga mbele. Kwa siku nzima, Emmanuel Macron atajikita kuwashawishi… pamoja na wakazi atakapowasili, viongozi waliochaguliwa katika baraza la idara… Tangu mwezi Desemba, ziara kadhaa za mawaziri zimefanyika, sheria ya dharura ya Mayotte imepitishwa, na sheria ya mageuzi iliyoahidiwa itawasilishwa jioni hii wakati wa mkutano wa Baraza la Mawaziri kwa njia ya video, ambapo Emmanuel Macron atakuwa mwenyekiti wa kikao hiki kutoka kwa ndege yake.
Ziara ya Emmanuel Macron inalenga kuonyesha kwamba anafuatilia suala hilo na kuanzisha “awamu ya ujenzi”, lakini pia kufanya maendeleo katika masuala nyeti sana ya usalama na uhamiaji haramu kutoka Comoro, ambayo ni kiini cha wasiwasi wa raia wa Mayotte.
Lakini ziara ya Emmanuel Macron haiko kwa Mayotte pekee. Bila shaka Rais wa Jamhuri anachukua fursa hiyo kwenda Réunion, ambayo ndiyo kwanza imekumbwa na Kimbunga Garance na inakabiliwa na janga kubwa la Chikungunya.
Wakati huo anatazamiwa kusafiri hadi Madagascar, ambako hakuna rais wa Ufaransa aliyefanya ziara ya nchi mbili tangu mwaka 2005, kuhudhuria mkutano wa kilele wa Kamisheni ya Bahari ya Hindi, kwa matumaini ya kuijumuisha Mayotte licha ya upinzani kutoka kwa Comoro.