TEC: Serikali ifanye mazungumzo na wadau wa uchaguzi, waliokamatwa waachiwe

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetoa wito kwa serikali ya Tanzania kuwaachilia mara moja na bila masharti viongozi wa kisiasa waliokamatwa kwa kudai haki, likisisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kulinda amani ya taifa, hasa kuelekea mwaka wa uchaguzi.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Wolfgang Pisa amesema ni muhimu Serikali kukaa na wadau wa uchaguzi, kuruhusu mabadiliko ya lazima kabla ya Uchaguzi Mkuu wa baadaye mwaka huu, huku akisisitiza umuhimu wa amani kuelekea uchaguzi huo na kutaka wote waliokamatwa kwa kudai mageuzi ya mifumo ya uchaguzi waachiwe haraka na bila masharti.

Askofu Pisa ambaye pia ni Askofu wa wa Jimbo Katoliki la Lindi ametoa wito huo usiku wa kuamkia leo Jumapili Aprili 20, 2025 katika mahubiri ya misa ya mkesha wa pasaka iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Andrea Kaggwa, mkoani Lindi.

Askofu Pisa amesema sauti na vilio vya wengi vinapaswa kusikika na kusisitiza kwamba kasoro zilizojitokeza zinapaswa kurekebishwa haraka. Kukiwa na nia ya dhati kutoka kwa wahusika muda unatosha kabisa kufanya hayo marekebisho kabla ya uchanguzi mkuu.

“Katika hali ya kawaida nani anaharibu amani, anayetumia nguvu na kusisitiza uchaguzi uende anavyotaka yeye au yule anayesema jamani turudi mezani ili tuangalie mifumo yetu ya uchaguzi, kwani kwa mfumo wa sasa hauwezi kutupatia viongozi wa haki na wa kweli?”— amehoji Askofu Pisa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *