WBDL kitawaka, timu tano kupambana

MCHUANO kwa timu za wanawake utakuwa kwa klabu tano kati ya timu 11 zinazoshiriki Ligi ya Kikapu ya Wanawake Mkoa wa Dar es Salaam (WBDL).

Mchuano huo unatokana na maandalizi ya timu hizo pamoja na ubora wa wachezaji zilionao.

Timu hizo ni Jeshi Stars, Tausi Royals, JKT Stars, Vijana Queens na ile mpya ya The Reel Dream. Jeshi Stars ilianza maandalizi mapema kwa lengo la kujenga timu tangu Januari na baada ya hapo iliandaa bonaza ililolipa jina la Twalipo, ambapo ilizialika timu mbalimbali zinazoshiriki WBDL.

Timu hiyo inajivunia nyota wenye uwezo wa kufunga katika eneo moja la mitupo mitatu ambao ni Ummy Yusuph, Anamary, Faraja Malaki, Witness Mapunda na Monalisa Kaijage.

Ti-mu ya Tausi Royals inayofanya mazoezi katika Uwanja wa Shule ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DIA) inajivunia  nyota wake Diana Mwendi, Juliana Sambwe, Tukusubira Mwalusamba na Tumaini Ndossi.  Nayo timu JKT Stars inatarajiwa kuwa mastaa wake wenye uwezo mkubwa ambao ni Jesca Ngisaise, Sara Budodi, Wade Jaha na Judith Nyari – wanaoweza kutupia  kutoka maeneo tofauti ya uwanja.

Nayo The Reel Dream iliyoanzishwa mwaka huu imesajili wachezaji wazoefu WBDL wakiwamo Rashda Zimbwe, Yassoda, Namukasa, Chikawe, Husna na Lydia wanaofundishwa na kocha mkongwe Dassy Makula. Timu nyingine ni Vijana Queens ambayo katika ligi ya mwaka huu imewapandisha daraja wachezaji wa kikosi cha pili cha City Queens baada ya kuondokewa na nyota wake na wamekuwa wakiuwasha katika viwanja vya mazoezi kwa ajili ya maandalizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *