Chad: Makumi ya wafungwa watoroka gereza la Mongo

Karibu wafungwa mia moja wametoroka gereza la Mongo, mji ulio katikati mwa Chad, katika jimbo la Guéra. Tukio hilo lilitokea Jioni ya Ijumaa Aprili 18. Kufikia sasa tumepokea habari chache kuhusu tukio hilo. Inaonekana kuwa watu kadhaa walifariki katika jela hilo wakati wa makabiliano kati ya wafungwa na walinzi wa gereza na wengine walijeruhiwa.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Dalili za kwanza za machafuko zilianza karibu 3:20 usiku siku ya Ijumaa, Aprili 18, katika gereza la Mongo, katikati mwa Chad. Kwa mujibu wa chanzo kwenye eneo la tukio kilichowasiliana na shirika la habari la AFP, wafungwa hao kwanza walishambulia ofisi ya mkuu wa gereza, kabla ya kukamata silaha zilizohifadhiwa humo. Kisha majibizano ya risasi yakatokea kati ya walinzi na baadhi ya wafungwa. Alipoarifiwa, gavana wa jimbo hilo, Abdoulaye Ibrahim Siam, mara moja alienda eneo la tukio. Kulingana na ripoti nyingi za vyombo vya habari, alikuwa mmoja wa watu watatu waliopigwa risasi na kujeruhiwa wakati wa makabiliano hayo.

Kulingana na ripoti ya muda kutoka tovuti ya habari ya Tchad Info, watu wanne walifariki wakati wa makabiliano hayo, na wengine 132 walichukua fursa hiyo kutoroka, “wafungwa wote wa makosa makubwa,” afisa wa utawala katika mji wa Mongo amesema. “Idadi ambayo imezua utata,” anaonya Waziri wa Sheria wa Chad Youssouf Tom, ambaye ametaka takwimu hizo kuthibitishwa kabla ya kuzungumza. Kwa mujibu wa waziri huyo, mwendesha mashitaka wa eneo hilo alikwenda katika eneo la tukio ili kuhakiki wafungwa  ambao bado wapo, ili kuweza kupata orodha ya wazi ya waliotoroka na sababu za makabiliano hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *