
Nchini Sudani, mashambulizi mapya yaliyozinduliwa siku ya Jumatano, Aprili 16, na Kikosi cha Msaada wa Haraka cha Jenerali Hemedti dhidi ya mji wa El-Fasher, ambao umezingirwa kwa mwaka mmoja, yamesababisha, kulingana na vyanzo vya matibabu, karibu vifo vya raia sitini na makumi ya wengine kujeruhiwa. Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) kililenga maeneo ya makazi ya jiji kwa silaha nzito. Jeshi la Sudani, kwa upande wake, linadai kuwa limesababisha hasara kubwa kwa FSR.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Mapigano kati ya jeshi la serikali na wanamgambo yalifanyika kusini mashariki na kaskazini mwa El-Fasher nchini Sudani. Miongoni mwa wahasiriwa ni watoto 15 na wanawake 17. Kulingana na Mtandao wa Madaktari wa Sudani, Kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) kilishambulia kwa makusudi msikiti mmoja ambapo watu tisa waliuawa, akiwemo mwanajiolojia mashuhuri.
Jeshi na vikosi vinavolisaidia vilizima shambulio hili mbaya la FSR, taarifa imesema, wakati likisema kuwa lilisababisha hasara kubwa kwa washambuliaji: makumi ya waliouawa na waliojeruhiwa pamoja na hasara ya vifaa vya kijeshi.
El-Fasher katikati mwa mashambulizi ya FSR
Shambulio hili linakuja chini ya wiki moja baada ya mashambulizi ya RSF dhidi ya kambi ya Zamzam karibu na El-Fasher, iliyo chini ya udhibiti wao. Kulingana na vyanzo kadhaa, kulikuwa na kati ya majeruhi 500 na 1,000 wa kiraia huko Zamzam, watu elfu moja walitoweka na maelfu kukimbia makazi yao.
Baada ya kupoteza Khartoum, wanamgambo wamezidisha mashambulizi yao huko Darfur Kaskazini. El-Fasher ni mji mkuu wa mwisho wa mkoa ulio nje ya udhibiti wao huko Darfur.
Katika taarifa mpya, kaka wa Hemedti na makamu wa rais wa RSF inayoongoza mapigano huko El-Fasher, Abderrahim Daglo, aliahidi kuuteka mji huo haraka, huku jeshi hilo kwa upande mwingine likidai kusitisha mapigano haraka iwezekanavyo.