
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mafuriko yaliua watu 33 mapema mwezi huu huko Kinshasa. Lakini kwa nini yalikuwa makali sana? Wakati huu, wanasayansi kutoka Shirika la Hali ya Hewa Ulimwenguni hawakuweza kuamua ikiwa, na kwa kiwango gani, ongezeko la joto duniani lilihusika. Hata hivyo, wanasayansi wana uhakika kwamba mji mkuu wa DRC haujazoea vya kutosha kukabiliana na hatari hii.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Mvua kubwa iliyosababisha mafuriko ya Aprili 4 huenda ikaudia kila baada ya miaka miwili, kulingana na Joyce Kimitai, mwandishi mwenza wa utafiti huo. Kwa hiyo ni muhimu kwamba jiji lijitayarishe kwa zana za ufuatiliaji wa hali ya hewa.
“Moja ya vipaumbele ni kuwekeza kwenye vituo vya hali ya hewa kwa ufanisi kwa sababu tumeona kuna mapungufu katika takwimu zilizopimwa na vituo vilivyopo. “Pia tunahitaji wafanyakazi zaidi kuzifuatilia,” amesema.
Hata hivyo, wanasayansi hawawezi kubainisha iwapo ongezeko la joto duniani linahusika na mafuriko ya hivi majuzi kutokana na ukosefu wa data.
“Hatuna usimamizi mzuri wa nafasi”
Ujenzi katika maeneo yanayokumbwa na mafuriko, uharibifu wa udongo kutokana na ukataji miti, mitandao ya mifereji ya maji isiyo na tija… Kinshasa haiko tayari kukabiliana na mafuriko haya, anasema Dieudonne Nsadisa Faka, mmoja wa waandishi: “Hatuna usimamizi wa busara wa nafasi katika suala la ugawaji wa ardhi, katika suala la mipango miji. Tunahitaji kurejea kutumia sayansi kama chombo cha maamuzi.”
Maamuzi haya yatalazimika kuzingatia kasi ya ongezeko la watu nchini DRC, wanasayansi wanatukumbusha. Idadi ya wakaazi wa Kinshasa, milioni 18 hivi leo, inatarajiwa kuongezeka maradufu ndani ya miaka 20.