Marco Rubio abaini kuwa Marekani inaweza kujiondoa katika juhudi za amani nchini Ukraine

Kabla ya kuondoka Paris, ambako ujumbe kutoka Marekani, Ukraine na nchi za Ulaya walikuwa wakikutana kujaribu kuratibu dhidi ya Vladimir Putin, Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio amebaini kwamba Washington inaweza kujiondoa katika juhudi za amani nchini Ukraine ikiwa mazungumzo yataendelea kukwama.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Marekani ina vipaumbele vingine” kuliko Ukraine. Huu ndio ujumbe Marco Rubio almewasilisha siku moja baada ya mkutano wa Paris kati ya nchi za Ulaya, Ukraine na Marekani: “Lazima tuamue katika siku zijazo ikiwa (amani) inawezekana au la,” na “ikiwa haiwezekani, lazima tuendelee, kwa sababu Marekani ina vipaumbele vingine,” amewaambia waandishi wa habari wachache kabla ya kuingia katika ndege yake kwenye uwanja wa ndege wa Le Bourget huko Paris.

Rais wa Marekani Donald Trump “alitumia siku 87 katika ngazi ya juu zaidi ya serikali yake akizidisha juhudi za kumaliza vita hivi,” huku akiwa amewapa wajumbe wake siku 100 kufikia lengo hili, ameongeza.

Takriban miezi mitatu baada ya kuwasili katika Ikulu ya White House, Donald Trump anatayarisha mawazo kwa ajili ya kumalizika kwa mazungumzo ya kusitisha mapigano nchini Ukraine.

Tutafanya tuwezavyo… Tutakuwa tayari kukusaidia unapokuwa tayari kufanya amani, lakini hatutaendelea na jitihada hii kwa wiki na miezi kadhaa. Kwa hivyo tunahitaji kuamua haraka sana, na ninazungumza juu ya siku chache, ikiwa hii inawezekana au la katika wiki chache zijazo. Ikiwa ndivyo, tuko tayari. Ikiwa sivyo, tunapaswa kuzingatia vipaumbele vingine …

“Nadhani Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zinaweza kutusaidia, kusonga mbele na kutuleta karibu na azimio. “Nimeona mawazo yao kuwa ya manufaa sana na yenye kujenga wakati wa majadiliano siku moja kabla na washirika wa Kyiv huko Paris,” amesema mkuu wa diplomasia ya Marekani. Marco Rubio amebainisha kwamba mzozo wa Urusi na Ukraine unafanyika “katika bara la Ulaya.”

Majadiliano yamekwama

Tangu kuapishwa kwake mwezi Januari mwaka huu, rais Trump amefanya maelewano na Vladimir Putin na anadai kuwa anafanya kazi kwa usitishaji wa haraka wa mapigano nchini Ukraine. Lakini majadiliano yanafanya maendeleo kidogo. Kyiv ilisalimu amri kwa shinikizo la Marekani kwa kukubali usitishaji vita wa siku 30 bila masharti, lakini Urusi ilifutilia mbali. Steve Witkoff, mjumbe maalum wa Trump, alikutana na rais wa Urusi kwa mara ya tatu mapema mwezi Aprili.

Kwa upande wao, Ufaransa na Uingereza zimeunda “muungano wa walio tayari” kuleta pamoja karibu nchi thelathini zinazoshirikiana na Ukraine. Muungano huu unafanya kazi hasa kuanzisha “kikosi cha uhakikisho” ili kuhakikisha uwezekano wa kusitisha mapigano na kuzuia uchokozi wowote mpya wa Urusi. Hata hivyo, wazo la kikosi cha kijeshi cha kimataifa katika tukio la makubaliano ya amani, inayotakiwa na Ukraine, bado halikubaliki kwa Moscow.

Kati ya Alhamisi, Aprili 17 na Ijumaa, Aprili 18, mashambulizi mapya ya Urusi yamepiga miji kadhaa mikubwa ya Ukraine, na kusababisha vifo vya watu wawili na majeruhi 40, kulingana na mamlaka ya Ukraine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *