Rwanda kuruhusu SAMIDRC kutumia ardhi yake kuingia Tanzania, duru za kidiplomasia zimesema

Rwanda imekubali kuruhusu wanajeshi waliotumwa na muungano wa Kusini mwa Afrika kupambana na waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kutoka mji unaoshikiliwa na waasi wa Goma kupitia ardhi yake hadi Tanzania, duru tatu za kidiplomasia zimesema siku ya  Ijumaa Aprili 18.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) yenye wanachama 16 ilisema katikati ya mwezi Machi imesitisha mamlaka hiyo na itaanza kuondoa kikosi chake kinachojulikana kama SAMIDRC, kutoka Kongo hatu kwa hatua.

Wanadiplomasia hao watatu, wakiwa na ufahamu wa mazungumzo yanayoendelea kati ya Rwanda na SADC, wamebainisha kwamba Rwanda imekubali ombi la askari wa kikosi hicho kupita nchini humo kwa njia ya ardhini.

Wawili kati ya wanadiplomasia hao wameongeza kuwa wamefahamishwa kuwa silaha za jeshi la kikanda zitafungwa kwa sababu za kiusalama lakini zitaondoka kupitia ardhi ya Rwanda na wanajeshi hao.

Hakukuwa na majibu ya haraka kutoka kwa SADC wala kutoka kwa wasemaji wa serikali ya Kongo na Rwanda walipoulizwa kutoa maoni yao.

Jenerali Rudzani Maphwanya, mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Afrika Kusini, amesema kwenye televisheni ya Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini siku ya Alhamisi kwamba timu ya kiufundi ilikuwa nchini Tanzania ikifanya kazi kwa undani zaidi kuhusu kuondolewa kwa wanajeshi wao.

SAMIDRC ilitumwa kusaidia Kinshasa kupambana dhidi ya makundi ya waasi katika maeneo ya mpakani ya mashariki ya Kongo yaliyoharibiwa na vita mnamo Desemba 2023.

M23 wameteka miji miwili mikubwa mashariki mwa Kongo tangu mwezi Januari katika kuongezeka kwa mzozo wa muda mrefu uliokita mizizi baada ya mauaji ya kimbari ya Kongo ya Rwanda mwaka 1994 na mapambano ya kudhibiti rasilimali kubwa ya madini ya Kongo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *