Makubaliano ya Madini: Kyiv na Washington zaia saini ‘mkataba wa Nia,’ Serikali yatangaza

Washington na Kyiv zimetia saini “mkataba wa dhamira” siku ya Alhamisi, Aprili 17, unaolenga kuhitimisha makubaliano tata kuhusu upatikanaji wa maliasili na madini muhimu ya Ukraine.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

“Tunafuraha kutangaza kutiwa saini, pamoja na mshirika wetu Marekani, kwa mkataba wa nia unaofungua njia kwa ajili ya makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi na kuundwa kwa Mfuko wa Uwekezaji wa Ujenzi Mpya wa Ukraine,” amesema Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine Yulia Svyrydenko kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Kyiv na Washington walikuwa wamepanga kusaini makubaliano juu ya uchimbaji wa madini ya kimkakati kutoka Ukraine wiki kadhaa zilizopita, lakini mzozo kati ya Rais Donald Trump na Volodymyr Zelensky mnamo mwezi wa Februari ulisitiisha kwa muda kazi ya makubaliano hayo.

Donald Trump anataka makubaliano hayo, ambayo yanalenga kuipa Marekani mrabaha wa faida kutokana na uchimbaji wa rasilimali za Ukraine na madini adimu, kuwa ni fidia ya msaada uliotolewa kwa Ukraine na mtangulizi wake, Joe Biden.

Yulia Svyrydenko hakutoa maelezo ya mkataba huo, lakini ameonyesha kuwa kazi ilikuwa ikiendelea kuelekea makubaliano ya mwisho.

“Zana ya ufanisi” kwa ajili ya ujenzi upya

“Tunatumai kuwa Mfuko utakuwa chombo madhubuti cha kuvutia uwekezaji katika ujenzi wa nchi yetu, uboreshaji wa miundombinu ya kisasa, msaada kwa biashara na uundaji wa fursa mpya za kiuchumi,” amebainisha.

“Kuna mengi ya kufanya, lakini kasi ya sasa na maendeleo makubwa yanatoa sababu ya kutumaini kuwa hati hiyo itakuwa ya manufaa kwa nchi zote mbili,” amesema Yulia Svyrydenko.

Maafisa wa Marekani wanasema kuimarisha maslahi ya kibiashara ya Marekani nchini Ukraine kutasaidia kuzuia Urusi dhidi ya uchokozi wa siku zijazo endapo kutakuwa na usitishaji vita.

Kyiv inadai dhamana thabiti ya kijeshi na usalama kama sehemu ya makubaliano yoyote ya kumaliza vita vya miaka mitatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *