
Waasi wa Houthi nchini Yemen wamesema leo Ijumaa, Aprili 18, kwamba mashambulizi mapya yaliyotekelezwa na Marekani kwenye bandari ya mafuta ya Bahari Nyekundu ya Ras Issa yamefikisha idadi ya vifo kuwa “20 na 50 kujeruhiwa,” kulingana na hesabu ya muda.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
“Idadi ya vifo kutokana na shambulio la Marekani kwenye bandari ya mafuta ya Ras Issa sasa inafikia 20,” amesema Anees Alasbahi, msemaji wa Wizara ya Afya ya Houthi. “Waokoaji watano na wahudumu wa afya wameuawa […] walipokuwa wakitekeleza wajibu wao,” chanzo hicho kimesema.
Mashambulio hayo ni mojawapo ya yale yaliyosababisha idadi kubwa zaidi ya vifo vya watu nchini Yemen, tangu Rais Donald Trump alipoanzisha kampeni ya kijeshi dhidi ya kundi la Wahouthi.
Kwenye taarifa yake, Jeshi la Marekani limesema vikosi vyake vimechukua hatua ya kusambaratisha chanzo cha mafuta kinachotumiwa na waasi wa Houthi. Limesema mashambulizi hayo yatawanyima waasi hao mapato yaliyowezesha kufadhili shughuli za waasi wa Houthi kwa zaidi ya miaka 10.