
Ingawa umepigwa marufuku nchini humo tangu 2015, ukeketaji ni mada ya mjadala tena nchini Gambia. Wiki hii, mahakama ya juu zaidi ya Gambia ilijitangaza kuwa na uwezo wa kuchunguza malalamiko yaliyowasilishwa na mbunge na vyama kadhaa vya kidini vinavyotaka kuharamisha tabia hii.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Mahakama ya Juu zaidi ya Gambia ilijitangaza kuwa na uwezo siku ya Jumanne, Aprili 15, kuchunguza malalamiko dhidi ya marufuku ya ukeketaji iliyowasilishwa na mbunge na vyama kadhaa vinavyotaka kuuharamisha.
Marufuku ya tabia hii imeanza kutumika nchini tangu mwaka 2015. Ili kuhalalisha hatua hiyo, dikteta wa zamani Yahya Jammeh – ambaye sasa anaishi uhamishoni – alibainisha “kutokuwepo kwa uhalali wa kidini [kwa ukeketaji] katika Uislamu.”
Ukweli unabaki kuwa licha ya sheria hii, ukeketaji haujawahi kutokomezwa nchini Gambia, ambayo ni mojawapo ya nchi kumi zilizo na kiwango kikubwa cha ukeketaji wa wanawake (FGM): 73% ya wanawake na wasichana wenye umri wa miaka 15 hadi 49 wamefanyiwa kitendo hiki, kulingana na takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) za mwak 2024.
Hata hivyo tangu mwaka jana, majaribio ya kuiondoa tena tabia hii yamekuwa yakiongezeka. Tayari mnamo mwezi Julai 2024, Mbunge Almameh Gibba – ambaye pia ni miongoni mwa waliowasilisha malalamiko mbele ya Mahakama ya Juu – aliwasilisha mswada wa athari hii, akisema kwamba marufuku ya ukeketaji “inakiuka haki za raia kutekeleza utamaduni na dini zao.”
“Je, watu wanaopeperusha bendera ya Kiislamu waliona wapi kwenye Quran kwamba wanawake wa Kiislamu wanatakiwa kutahiriwa”,
Mame Sira Konaté, Katibu Mkuu wa Muungano wa Wanawake wa Kiafrika dhidi ya Ukeketaji na Unyanyasaji unaohusiana na Mila.
Ingawa hatimaye ilikataliwa, maandishi hayo hata hivyo yalizua mzozo mkali na kugawanya sana nchi hiyo yenye Waislamu wengi. Katika maandamano, karibu wanawake mia moja na “walionusurika,” kama waathiriwa wa ukeketaji wanavyojieleza, walikusanyika mbele ya Bunge la taifa.
Wanaharakati wa kupinga ukeketaji na Umoja wa Mataifa, kwa upande wao, wanasisitiza kuwa ukataji ni mila inayokiuka haki za binadamu. Kando na maumivu na kiwewe kinachosababishwa, inaweza kuwa na athari zingine mbaya: maambukizo, kutokwa na damu, na baadaye utasa na shida wakati au baada ya kuzaa.