
Kundi la Hamas sasa linataka kuwepo kwa makubaliano ya kina ya kumaliza vita huko Gaza na kubadilishana mateka wote kwa Wapalestina waliofungwa nchini Israel, afisa mkuu wa kundi hilo amethibitisha huku akikataa pendekezo la Israeli kusitisha mapigano kwa muda.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Kundi hilo linasema halitokubali makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda, likidai Israel inalenga kutumia maafikiano ya aina hiyo kuendelea kutekeleza uharibifu kwenye Ukanda wa Gaza.
Hamas inasisitiza kuwa, inataka kuwaachia mateka wote wa Israel kwa kubadilishana na raia wake wanaoshikiliwa katika jela za Israel.
Wapatanishi kutoka Misri na Qatar, wamekuwa wakijaribu kutafuta makubaliano kama yale yaliopelekea kusitishwa kwa mapigano mwezi Januari mwaka huu bila ya hata hivyo kufikia lengo lao.
Israel na Hamas zimekuwa zikiendelea kutuhumiana kwa uvujifu wa makubaliano ya kusitisha mapigano, kila mmoja akimtuhumu mwengine kwa kuanzisha mashambulio.