Wawakilishi kutoka mataifa ambayo yanashirikiana kwa karibu na Ukraine, wanakutana jijini Paris nchini Ufaransa, kujadiliana namna ya kusaidia nchi hiyo kupata amani.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Mkutano huu ambao mwenyeji wake ni rais Emmanuel Macron, ambao unahudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio, na Steve Witkoff mjumbe maalum wa rais Donald Trump, unakuja wakati huu, shinikizo za Washington za kusitisha vita kati ya Urusi na Ukraine, zikiendelea kugonga mwamba.
Rais Trump, tayari ameonesha masikitiko yake, kutokana na msimamo mgumu wa rais Vladimir Putin, ambaye amekataa kuunga mkono pendekezo lililokubaliwa na Ukraine, la kusitisha vita hivyo kwa angalau siku 30 ili kutoa fursa ya majadiliano.
Rais wa Ukraine, Vlodymr Zelensky amewaambia washirika wake wanaokutana kwenye kikao cha Paris, kuangalia namna ya kuendelea kuishinikiza Urusi, kukubali mkataba wa usitishwaji vita.
Urusi, kwa upande wake kupita Dmitry Peskov, msemaji wa rais Putin, amepuuzilia mbali mkutano wa Paris na kusema hautakuja na suluhu na badala yake vita vitaendelea.
Ufaransa inasema lengo la mazungumo hao ni kuthathmini, jitihada zinazofanyika, kusitisha vita vinavyoendelea kwa mwaka wa tatu sasa.