
Wapiganaji wa kiislamu wa kundi la Al Shaabab nchini Somalia, hapo jana waliripotiwa kushambulia mji muhimu unaotuimiwa na serikali kuratibu operesheni za kijeshi dhidi ya kundi hilo, hatua inayokuja wakati huu kundi hilo likiendelea kuchukua vijiji zaidi vilivyokaribu na Mogadishu.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Vyanzo kutoka eneo hilo la katikati mwa Somalia vimethibitisha kuwa wapiganaji hao wameanza kusonga mbele katika harakati zao baada ya hivi karibuni kuteka vijiji kadhaa vilivyoko umbali wa kilomita 50 (maili 30) kutoka mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Kwa mujibu wa taarifa za kiintelijensia ni kuwa kundi hilo lenye kufungamana na al Qaeda, linalenga mji a Mogadishu, Hata hivyo afisa wa kijeshi katika mji wa Adan Yabaal, Kapteni Hussein Olow, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba wanajeshi wa serikali wamewarudisha nyuma.
Wanamgambo hao walianzisha mashambulio dhidi ya vituo vya jeshi la Somalia katika wilaya ya Adan Yabaal asubuhi ya jan ambapo Kulikuwa na mapigano makali ambayo bado yanaendelea katika baadhi ya maeneo, alisema afisa huyo wa jeshi la Somalia, na kuthibitisha kuwa usalama umeimarishwa kuzuia wanamgambo hao wa Al Shabaab.