
Iran “haiko mbali” na kuwa na bomu la atomiki, ameonya mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA), katika mahojiano na Gazeti la kila siku la Ufaransa Le Monde yaliyochapishwa Jumatano, Aprili 16, saa chache kabla ya ziara yake huko Tehran.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
“Ni kama fumbo, wana vipande na siku moja wanaweza kuviweka pamoja. Bado kuna safari ndefu kabla ya kufika huko. Lakini hawako mbali na kuwa na bomu hilo, lazima tutambue hilo,” amesema. “Haitoshi kuiambia jumuiya ya kimataifa ‘hatuna silaha za nyuklia’ ili wakuamini. “Tunahitaji kuwa na uwezo wa kuthibitisha,” ameongeza.
“Ingawa Iran ina nyenzo za kutosha kutengeneza mabomu kadhaa, bado haina silaha ya nyuklia. Lakini haiko mbali na kuwa nalo “, amebainisha.
Mkuu wa shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki amesisitiza nia yake ya kuona shirika lake likishirikishwa katika mazungumzo yaliyoanzishwa nchini Oman kati ya Iran na Marekani kuhusu suala la nyuklia ya Iran.