Kenya: Uchunguzi kuhusu upandikizi wa figo waanzishwa dhidi ya hospitali moja

Nchini Kenya, Wizara ya afya imeagiza uchunguzi kwenye hospital ya kibinfasi ya Mediheal iliyopo jijini Eldoret, inavyoendesha huduma ya kupandikiza wagonjwa figo, baada ya ripoti kuwa inahusika na biashara haramu ya uuzaji wa viungo vya binadamu.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa afya Aden Duale, ameagiza pia uchunguzi katika vituo saba nchini Kenya vinavyojihusisha na upandikizi wa figo ili kubaini iwapo kuna biashara haramu inayoendelea.

Agizo la uchunguzi, pia linakuja baada ya mwaka 2023, ripoti ya kamati maalum ya Wizara ya afya kuhoji hatua ya hospitali hiyo kufanya upandikizi wa figo 372 kwa kipindi cha miaka mitano, hali iliyoelezwa sio ya kawaida, na kutaka uchunguzi zaidi kufanywa.

Hatua hii inakuja baada ya ripoti ya kiuchunguzi kutoka mashirika ya Habari ya Ujerumani ikiwemo Deutsche Welle , katika ripoti ya kiuchunguzi kubaini kuwa , vijana wasio na ajira nchini Kenya na watu wengine  wamekuwa wakishawishiwa kuuza figo zao kwa ajili ya kupata fedha na hospitali ya Mediheal.

Aidha, imeripotiwa kuwa,  wagongwa kutoka Israeli na Ujeurumani wamekuwa wakipata huduma hiyo kwenye hospitali hiyo na kuzua maswali ni kwa nini waliamua kupata huduma hiyo nchini Kenya na sio kwenye nchi zao, zilizoendelea.

Baadhi ya watu  waliotoa figo zao, hawakupewa taarifa za kina na kueleweka kuhusu hatua hiyo na kulipwa kiasi kidogo cha fedha kinyume na waliovyokubaliana na uongozi wa hopsitali ya Mediheal jijini Eldoret kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Hata hivyo, uongozi wa Mediheal, umekanusha ripoti hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *