Mchezaji wa zamani wa Girondins ya Bordeaux afariki nchini China, akiwa na umri wa miaka 28

Habari ya kusikitisha kwa soka la Gabon. Aaron Boupendza amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 28, Shirikisho la Soka la Gabon limetangaza Jumatano, Aprili 16. Mshambulizi huyo, ambaye alichezea klabu kadhaa za Ufaransa kama vile Bordeaux, Pau na Tours, alikuwa akicheza nchini China katika klabu ya Zhejiang FC.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na ripoti kutoka vyombo vya habari vya Romania kama vile Fanatik na TVR Info, Aaron Boupendza, mchezaji wa kimataifa wa Gabon ambaye amecheza mara 35 na kufunga mabao nane, alianguka kutoka ghorofa ya 11 ya jengo nchini China. Kulingana na vyanzo hivi, uchunguzi unaendelea na mamlaka pia inazingatia uwezekano wa kujiua.

Baada ya kuhamia Uturuki msimu wa 2020/2021 ambapo alifunga mabao 22 akiichezea klabu ya Hatayspor, Aaron Boupendza kisha alichezea vilabu vya nchi kadhaa kama vile Qatar, Saudi Arabia, Marekani na Romania kabla ya kutua China mwezi Januari mwaka huu. Baada ya kukaa kwa muda wa miezi 18 katika klabu ya Rapid Bucharest nchini Romania, kocha wake wa zamani, Marius Sumudica, amethibitisha habari hizo za kusikitisha kwa vyombo vya habari vya GSP.

Akiwa amewasili Bordeaux kutoka klabu ya Gabon CF Mounana mnamo 2016, Aaron Boupendza hajawahi kuvaa jezi ya Girondins. Alitumia mkopo mfululizo katika Pau, Gazélec d’Ajaccio, Tours na klabu ya Ureno ya Feirense.

Alisimamishwa na Girondins kwa “tabia isiyofaa na tabia isiyoendana na maadili ya kilabu”, kabla ya kuondoka kilabu hiyo kwenda Uturuki na kuwa na msimu bora zaidi wa maisha yake huko.

Mchezaji wa kimataifa tangu 2016 akiwa na Gabon, alishiriki kwenye Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya mwaka 2021 ambapo Panthers waliondolewa kwenye hatua ya mtoano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *