Uingereza: Ufafanuzi wa kisheria wa mwanamke unategemea jinsia ya kibaolojia

Mahakama ya Juu ya Uingereza imetoa uamuzi Jumatano, Aprili 16, kuhusu ufafanuzi wa kisheria wa mwanamke. Inategemea jinsia ya kibaolojia, sio jinsia, uamuzi ambao unaweza kuwa na matokeo kwa wanawake waliobadili jinsia.

Imechapishwa:

Dakika 3

Matangazo ya kibiashara

Ufafanuzi wa kisheria wa mwanamke unatokana na jinsia ya kibayolojia, sio jinsia, Mahakama ya Juu ya Uingereza imeamua siku ya Jumatano, Aprili 16, katika uamuzi nyeti sana ambao unaweza kuwa na madhara makubwa kwa wanawake waliobadili jinsia nchini Uingereza.

Mzozo huo umekuwa ukiendelea tangu mwaka2018 kati ya serikali ya Scotland, ambayo imejitolea sana kwa haki za watu waliobadili jinsia katika miaka ya hivi karibuni, na chama cha wanawake “For Women Scotland.”

“Uamuzi wa pamoja wa Mahakama hii ni kwamba maneno ‘mwanamke’ na ‘jinsia’ katika Sheria ya Usawa ya mwaka 2010 yanarejelea mwanamke wa kibaolojia na jinsia ya kibayolojia,” wameamua majaji wa mahakama ya juu zaidi ya Uingereza.

Mahakama ya Juu, hata hivyo, imehakikisha kwamba watu waliobadili jinsia wamelindwa na sheria hii, “sio tu dhidi ya ubaguzi kupitia sifa inayolindwa ya ubadilishaji wa jinsia, lakini pia dhidi ya ubaguzi wa moja kwa moja, ubaguzi usio wa moja kwa moja na unyanyasaji unaohusiana na jinsia yao waliyopata.”

“Ni siku nzuri”

Uamuzi huo umepokelewa kwa shangwe kutoka kwa makumi ya wanaharakati wa For Women Scotland. “Ninatetemeka (…) Ni siku nzuri,” amejibu mmoja wao.

“Tumefikiri kwamba haki za wanawake zingerudi nyuma, na leo majaji wamesema kile ambacho tumeamini siku zote: wanawake wanalindwa na jinsia yao ya kibaolojia,” amesema Susan Smith, mkurugenzi mwenza wa chama hicho.

“Wanawake sasa wanaweza kujisikia salama wakijua kuwa huduma na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya wanawake yamewekwa kwa ajili ya wanawake,” ameongeza.

Kwa upande wao, vyama vya LGBT+ vilikuwa vimeelezea hofu kabla ya uamuzi kwamba wanawake waliobadili jinsia hawataweza tena kufikia baadhi ya maeneo, ikiwa ni pamoja na kituo cha wanawake.

Sheria ya 2010 katika kiini cha mjadala

Ni suala lenye mgawanyiko mkubwa, na kuzua mzozo mkali kati ya watetezi wa haki za binadamu na wanaharakati ambao wanabaini kwamba baadhi ya madai yao yanatishia haki za wanawake.

Kiini cha mjadala huo kilikuwa tafsiri ya Sheria ya Usawa ya Uingereza ya mwaka2010. Kwa mujibu wa serikali ya Scotland, maandishi haya yalikuwa wazi: ikiwa mwanamke aliyebadili jinsia amepata Cheti cha Kutambua Jinsia (GRC) kufuatia mabadiliko yake, anachukuliwa kuwa mwanamke na ana haki ya “ulinzi sawa na wale waliotangazwa wanamke wakati wa kuzaliwa.”

Kwa jumla, baadhi ya watu 8,500 wamepata cheti cha GRC nchini Uingereza tangu mpango huo ulipoanzishwa mwaka 2004, serikali ya Scotland ilisema mwezi Novemba.

Suala tata Scotland

Uamuzi wa Mahakama ya Juu unaweza kusikizwa hata nchini Marekani. Tangu arejee Ikulu ya Marekani mwezi Januari, Donald Trump amelenga watu waliobadili jinsia, ikiwa ni pamoja na mipango ya kuwafukuza jeshini na kuzuia taratibu za mpito kwa wale walio chini ya miaka 19.

Wahafidhina wa Uingereza, ambao walishindwa katika uchaguzi mkuu katika majira ya kiangazi ya mwaka 2024, walikuwa wameahidi, ikiwa wangeshinda, wangefanya “ufafanuzi” katika sheria ili neno “jinsia” liwe tu kwa jinsia ya kibaolojia.

Suala hili daima limekuwa tata hasa huko Scotland. Mnamo mnamo mwaka 2022, serikali ya Scotland ilipitisha sheria ya kuwezesha ugawaji upya wa jinsia bila ushauri wa matibabu, kuanzia umri wa miaka 16. Maandishi haya yalikuwa yamezuiwa na serikali ya Conservative huko London.

Mnamo Januari 2023, mamlaka ya Scotland pia ilitangaza kusimamishwa kwa uhamisho wa mfungwa yeyote aliyebadili jinsia ambaye ana historia ya unyanyasaji dhidi ya wanawake hadi kwenye gereza la wanawake, kufuatia kesi mbili ambazo zilichochea hasira umma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *