
Rais wa Togo Faure Gnassingbé, ambaye ni mpatanishi mpya wa mzozo kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda, anazuru Kinshasa, ikiwa ni ziara ya kwanza, baada ya kuteuliwa katika nafasi hiyo.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
ZIara yake inakuja baada ya kutangazwa kuwa mpatanishi mpya, na mtangulizi wake, rais wa Angola João Lourenço, ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika.
Baada ya kumkabidhi kijiti, Lourenço, ambaye amekuwa mpatanishi tangu mwaka wa 2022, amemwondoa Brigedia Daniel Raimundo Savihemba, ambaye amekuwa akiongoza Kamati maalum, kusimamia mchakato wa Luanda kujaribu, kusaidia kuleta amani Mashariki mwa DRC.
Licha ya kupewa jukumu la kuwa mpatanishi, Umoja wa Afrika, haujaweka majukumu yake, baada ya jitihada za kidiplomasia za mpatanishi aliyetangua kutozaa matunda.
Kabla ya kwenda Kinshasa, rais huyo wa Togo, amekutana na rais Lourenço, jijini Luanda.
Wachambuzi wa siasa na masuala ya diplomasia wanasema, Gnassingbé, anakuja kwenye mzozo huu, akiwa hana upande kwa sababu Togo, sio mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, au SADC na huenda umbali wa nchi yake na DRC na Rwanda huenda ikasaidia.