Nchi wanachama wa WHO zakubaliana na ya kushirikiana wakati wa majanga

Nchi wanachama wa Shirika la afya duniani WHO, zimekubaliana utaratibu wa namna ya kukabiliana na majanga makubwa ya magonjwa katika siku zijazo, ili kuepuka changamoto zilizozuka baada ya mlipuko wa Uviko 19.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Makubaliano hayo, yamefikiwa na wawakilishi wa nchi mbalimbali, baada  ya miaka mitatu ya majadiliano.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema hatua hiyo ni muhimu, kuhakikisha kuwa dunia inakuwa salama.

Mwafaka huo pia umekuja, baada ya nchi wanachama hapo awali kushindwa kukubaliana kuhusu masuala nyeti hasa nafasi ya teknolojia kwenye kukabiliana na milipuko ya magonjwa katika siku zijazo na athari yake kwa mataifa masikini.

Kikubwa katika makubaliano hayo ni kuwa nchi tajiri na kampuni zinazotenegeza dawa na chanjo, zitaweka wazi taarifa na mbinu za kusaidia kupambana na magonjwa pindi tu yanapolipuka.

Wakati wa janga la UVIKO 19 ambapo mamilioni ya watu walipoteza maisha kote duniani, mataifa masikini yaliyashtumu yale tajiri kwa kuficha chanjo na vifaa vya kufanya vipimo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *