Wakali wa hat trick fa maguri, shaibu wamo

WAKATI mashindano ya Kombe la Shirikisho (FA) yakitinga hatua ya nusu fainali, nyota kadhaa wamefunga ha trick katika mechi walizocheza, huku wale wa Ligi ya Championship wakitamba.

Nyota wa kwanza kufunga hat trick ni Kassim Shaibu ‘Mayele’ wa TMA Stars waliposhinda mabao 5-1 dhidi ya Mabingwa wa Mkoa wa Tanga, Leopards FC hatua ya 64 bora kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Desemba 5, 2024.

Mwingine ni Elias Maguri anayeichezea kwa sasa Geita Gold aliyeifungia Biashara United katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya TRA ya Kilimanjaro katika hatua hiyo kwenye Uwanja wa Karume Musoma, Desemba 7, 2024.

Nyota mwingine ni Raizin Hafidh wa Mtibwa Sugar aliyefunga ikishinda mabao 5-3 dhidi ya mabingwa wa Mkoa wa Singida, Town Stars hatua ya 32 bora kwenye Uwanja wa Manungu Complex, Morogoro Machi 3, 2025.

Kwa upande wa timu za Ligi Kuu,

mabao manne aliyofunga kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz KI katika ushindi wa 8-1 dhidi ya Stand United, juzi kwenye robo fainali yalimfanya kuwa mchezaji pekee wa ligi hiyo kufunga hat trick katika FA msimu huu.

Aziz KI alifunga mabao hayo katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa KMC Complex na kuipeleka Yanga  nusu fainali ambapo sasa itacheza na JKT Tanzania iliyoichapa Pamba Jiji 3-1.

Tangu michuano ya Kombe la Shirikisho (FA) ianze msimu huu, Aziz KI ndiye mchezaji pekee wa Ligi Kuu aliyefunga ‘hat-trick’, huku nyingine tatu kati ya nne zilizofungwa zikiwekwa kambani na mastaa kutoka Ligi ya Championship, tofauti na msimu uliopita.

Rekodi hiyo imeivuka ile ya msimu uliopita kwani ni nyota wawili wa Ligi ya Championship waliofunga hat trick kati ya saba zilizofungwa ambao ni Pascas Wagana anayeichezea Biashara United ya Mara na Shaban Seif wa Mbuni FC ya Arusha.

Katika hat trick saba za msimu uliopita, tano zilikuwa za mastaa wa Ligi Kuu kina Edward Songo wa JKT Tanzania, Kelvin Sabato (Namungo FC), Yohana Nkomola (Tabora United), Clement Mzize (Yanga) na Sadio Kanoute (Simba). Baadhi ya nyota wa timu hizo wana nafasi ya kuongeza idadi kutokana na timu zao kutinga nusu fainali ambazo ni Simba, Yanga, Singida Black Stars na JKT Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *