Ushuru wa forodha: Idara ya Posta ya Hong Kong yasitisha kutuma vifurushi kwa Marekani

Idara ya Posta ya Hong Kong imetangaza siku ya Jumatano, Aprili 16, kwamba inasitisha usafirishaji wa vifurushi kwenda Marekani ili kujibu nyongeza ya “kutisha” ya ushuru ya Rais wa Marekani Donald Trump.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake, idara ya Posta imesema kwamba itaacha “kukubali bidhaa za barua zilizo na bidhaa” zinazotumwa kwenda Marekani. Hatua hii itaanza kutumika mara moja kwa barua zinazotumwa kwa njia ya bahari na itaanza kutumika Aprili 27 kwa njia ya anga.

Donald Trump alitia saini agizo la utendaji wiki iliyopita linalositisha misamaha ya ushuru kwenye vifurushi vidogo vilivyotumwa kutoka China, kama vile vile vilivyotumwa na makampuni makubwa ya biashara ya mtandaoni Shein na Temu. China na Marekani zimeingia katika vita vya zabuni kuhusu ushuru wa forodha: Washington imetoza ushuru wa 145% kwa bidhaa za China zinazoingia katika eneo lake, pamoja na zile zilizokuwepo kabla ya Donald Trump kurejea White House. Beijing ilijibu kwa kiwango ambacho sasa kinasimama kwa 125%.

Agizo kuu la mwaka 2020 la Donald Trump liliondoa upendeleo kwa Hong Kong. Kwa hivyo, koloni la zamani la Uingereza pia limeathiriwa na ushuru wa ziada wa 145% uliowekwa kwa China. Kutoza ushuru wa forodha kwa Hong Kong “hakuna aibu sana,” Xia Baolong, mkurugenzi wa Ofisi ya Kazi ya Hong Kong na Macao, alishutumu siku moja kabla. Kiongiozi wa serikali ya Hong Kong John Lee pia amekosoa ushuru wa Marekani akiutaja kama “upuuzi,” akisema ushuru wowote unapaswa kuwa sifuri, kwani Hong Kong ni bandari huru. “Marekani haina busara, inanyanyasa na inatoza ushuru kwa njia isiyo ya haki,” idara ya posta ya Hong Kong pia imejibu siku ya Jumatano.

Kuhusu vifurushi ambavyo tayari vimetumwa lakini bado havijasafirishwa, idara ya Posta ya Hong Kong imebaini kwamba ingewasiliana na watumaji ili kuwarejeshea vifurishi vya na kuwarejeshea gharama za posta kuanzia Aprili 22. Barua hazihusiki, idara ya Posta ya Hong Kong imesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *