Kongamano la kuisaidia Sudan linafanyika nchini Uingereza

Wanadiplomasia kutoka katika nchi mbalimbali duniani wanakutana jijini London kwa kongamano la siku moja kujaribu kuchangisha fedha za kusaidia hali ya kibinadamu inayoendelea kuwa mbaya nchini Sudan.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Licha ya kongamano hilo kuandaliwa, wawakilishi wa jeshi la Sudan wala wapiganaji wa RSF hawakualikwa.

Mzozo wa Sudan ambao umeingia katika mwaka wa pili sasa, umesababisha vifo vya makumi kwa maelfu ya raia wakati watu wengine Milioni 14 wakipoteza makazi yao.

Mapiagano kati ya jeshi la wapiganaji wa RSF yamesababisha pia kutokea kwa baa kubwa zaidi la njaa nchini Sudan.

Abdel-Fattah Burhan anayeoongoza wanajeshi watiifu kwa serikali yake.
Abdel-Fattah Burhan anayeoongoza wanajeshi watiifu kwa serikali yake. AP

Kongamano hilo limeandaliwa kwa ushirikiano wa mwenyeji Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika.

Waandaaji wa kongamano hilo wanasisitiza kwamba nia yao ni kusaidia tu katika uchangisha wa fehda kusaidia Umoja wa Mataifa kushugulika hali ya kibinadamu inayoendelea Sudan.

Sudan ilitumbukia katika mapigano tarehe 15 ya mwezi Aprili mwaka wa 2023 kati ya wapiganaji wa RSF na wanajeshi wa watiifu kwa serikali.

Mwanamke akiwa na mtoto katika kambi ya wakimbizi ya Zamzam kaskazini mwa Darfur.
Mwanamke akiwa na mtoto katika kambi ya wakimbizi ya Zamzam kaskazini mwa Darfur. via REUTERS – Mohamed Zakaria

Makabiliano yalianzia katika Mji Mkuu Khartoum, kabla ya kusambaa katika maeneo mengine ya nchi,watu Elfu 20 wakirpotiwa kuuawa japokuwa huenda idadi hiyo ikawa kubwa.

Mwezi uliopita, wanajeshi wa serikali walitangaza kuchukua tena udhibiti wa Mji Mkuu Khartoum, ishara ya kwamba walikuwa wamepata ushindi dhidi ya mapigano yanayoendelea.

Soma piaWatoto waathirika pakubwa na mzozo wa miaka miwili Sudan: UNICEF

Kwa upande mwengine, wapiganaji wa RSF bado wanadhibiti sehemu kubwa ya Mji wa Darfur.

Shirika la mpango wa chakula katika Umoja wa Mataifa, WFP linasela karibia watu Milioni 25, nusu ya idadi ya raia wa Sudan wanakabiliwa na baa kubwa la njaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *